Mwandishi wa Sibuka afariki dunia kuzikwa
Alhamisi
NA Andrew Chale
MWANDISHI wa
Habari wa kituo cha SIBUKA, aliekuwa akitangaza na kuandaa vipindi
mbalimbali kikiwemo cha Pepeta Afrika, Lulu Oscar amefariki dunia jana Jumanne
nyumbani kwao Mbezi Kwa Yusufu.
Akizungumza na
.. mtandao/gazeti mdogo wa marehemu, Ritha Oscar alisema kuwa
Lulu alipatwa na mauti hayo majira ya usiku ambapo alizidiwa ghafla
kufuatia kulalamikia kifua kumbana.
“Awali alikuwa
amelazwa kwenye hospitali ya Masister ya Luguluni kule Mbezi,
zaidi ya mara tatu, jana aliruhusiw kurudi nyumbani lakini baada
ya kuendelea vizuri lakini jioni usuku alilalamikia kifua kikimbana
tulimuangaikia mpaka hatua ya mwisho lakini ikashindikana na alipoteza
maisha” alisema Ritha kwa masikitiko makubwa.
Ritha alisema
kuondoka kwa Lulu kwenye familia yao ni pigo kubwa kwani alikuwa bado ni mdogo
na alikuwa msaada mkubwa kwa ndugu na jamaa.
Aidha, alisema
kuwa, kikao cha muda cha ndugu kilichokaa wameafikiana kuzikwa siku ya Alhamisi
katika Makaburio ya Kinondoni. “Mpaka sasa taarifa za familia, ni kuwa mazishi
yatakuwa siku ya Alhamisi pale mkaburi ya Kinondoni na msafara utaanzia nyumbani
Mbezi kwa Yusufu na kuelekea Makaburini” alisema Ritha.
Marehemu
alikuwa mwajiliwa wa televisheni ya SIBUKA (TV SIBUKA) akiwa kama mtangazaji na
mwandaaji wa vipindi ambapo pia alikuwa akiandaa na kutangaza kipindi cha Pepeta
Afrika, kilichojizola umaarufu mkubwa mpaka anakufa kwake.
Katika historia
yake, Lulu alihitimu elimu yake ya msingi alihitimu
mwaka 1996 katika shule ya Upanga na kwa elimu ya uandishi wa habari alisomea
chuo cha Royal College of Tanzania na baadae mwaka 2003, aliweza
kuhitimu kozi zake hiyo ya juu katiika Taasisi ya uandishi wa habari na
mawasiliano Institute of journalisim and mass
communication.
Marehemu
alikuwa hajaolewa wala hajaacha mtoto.


Post a Comment