Vijana kutoka vyuo mbali mbali mkoani
Arusha wameshiriki katika semina ya biashara iliyotolewa na shirika la
wafanyakazi duniani (ILO) ikiwa ni njia mojawapo ya kuwajengea vijana
uwezo wa kujitegemea kiuchumi nje ya ajira.
Semina hiyo inalenga kutoa elimu na hamasa
kwa vijana juu ya namna ya kuingia katika soko la biashara na kunufaika na fursa
zilizoko katika soko hilo zitakazowawezesha kujikomboa kiuchumi na kuachana na
utegemezi hasa wakutegemea kuajiriwa.
Billy Mushi ni Mjasiriamali ambaye ni mtoa
mada anaeleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuingiza watu wapya kwenye biashara
hususani watu wa ngazi mbali mbali kutoka vyuoni,mashirika na benki na kuongeza
kuwa vijana wanapaswa kujua kwamba wananaweza kufanikiwa endapo watatumia mbinu
za kijasiriamali.
Tayari wameshatoa elimu hiyo kwa watu 1200
ambapo wanatoa mafunzo hayo si tu wale wenye uwezo wa kufundisha tu bali ni watu
wenye uzoefu na waliobobea katika soko la biashara hivyo wanafunisha njia
walizopitia ili kutoa hamasa kwa wengine kuthubutu kutumia fursa za kibiashara
zilizoko kwenye maeneo yao ili waweze kufanikiwa kiuchumi,kimaisha na kutimiza
ndoto zao.
Hata hivyo ametoa wito kwa vijana kushiriki
katika semina,warsha mbali mbali na mafunzo ya ujasiriamali ili kujijengea
uwezo,maarifa na mbinu za kufanikiwa kiuchumi ili kuondokana na
umasikini,utegemezi na tatizo sugu la ukosefu wa ajira linalowakabili vijana
wengi nchini.
Joseph Mayagila ni Mkurugenzi wa Mafunzo
katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) kilichoshiriki
katika mafunzo hayo anasema kuwa mafunzo hayo hayawaandaa wanafunzi kutegemea
mshahara tu bali yaawaandaa kufanikiwa kiuchumi aidi ya hapo ili mwanafunzi
anapohitimu chuo aweze kujimudu kiuchumi mbali na kutegemea ajira peke
yake.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa
mafunzo hayo yatawawezesha vijana kushiriki kiuchumi katika ulimwengu wa
digitali na kuabiliana na ushindani wa kimasoko.Hata hivyo wanafunzi wa huo
chake walioshiriki idadi ao ni 390 huku wanafunzi wengine kutoka Kilimanjaro
Film Institute (KFI).


Post a Comment