IMG 9338 Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles
Tizeba akisalimiana na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA),
wakati alipofanya ziara katika Kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam Leo, kujionea shughuli Mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Nyuma ya
Waziri wa Uchukuzi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi. Suleiman
Suleiman.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(mwenye
suti nyeusi) akiangalia eneo la Kipunguni B ambalo lilifanyiwa tathmini kwa
ajili ya kuongeza eneo la Kiwanja cha Ndege cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata
maelezo ya namna kituo cha hali ya Hewa kinavyofanya kazi katika utoaji wa
Taarifa mbalimbali za hali ya Hewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kutoka kwa Bi. Pamela Gabriel kutoka Mamlaka
ya Hali ya hewa Tanzania (TMA).Naibu Waziri wa Uchukuzi alifanya Ziara hiyo
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Uwanja huo
leo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata
malezo kutoka kwa Afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Elieza
Mwalutende, wakati Naibu Waziri huyo alipotemmbelea Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwl . Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa katika kiwanja hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba
(aliyeweka mikono miwili mfukoni) akipata maelezo ya namna kikosi cha zima Moto
katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere kinavyofanya kazi,Wakati wa Ziara
yake hii leo Katika uwanja Huo.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba (aliyeweka
mkono mfukoni) akipata maelezo ya namna Genereta za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzani(TAA) zinavyofanywa kazi endapo umeme utakatika kutoka kwa Bi. Rehema
Ahmed (mwenye Hijabu), wakati wa Ziara yake katika uwanja huo
leo.
Hayo ni Majenereta yanayotumika endapo Umeme wa
TANESCO unapokatika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijjini Dar es Salaam.
Post a Comment