JESHI la Polisi mkoani Mbeya
limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya mapenzi na
mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo
wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba
21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa
la wizi.
Kamanda Athumani alisema
kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya
Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito
kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi
kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho
ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia
sheria.
Akizungumzia tukio hilo,
baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha
kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi
ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali
zake.
Wakati huohuo, katika
kijiji cha Malangali Barabara ya Mbeya-Iringa, Wilaya ya Mbarali gari aina ya
Nissan Patrol lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo
hapo.
Alisema kuwa mwili wa
marehemu bado haujafamika na mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala
Mission na kwamba juhudi za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka
zinaendelea.
Post a Comment