Wachezaji wa timu ya
taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys wakishangilia bao
lililofungwa na Mudathiri Yahaya Abbas wakati timu hiyo ilipopambana na Congo
Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wenye
umri huo, zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Serengeti Boys imeshinda 1-0.
(Picha zote na Habari Mseto Blog)
Kocha Mkuu wa Serengeti
Boys, Jacob Michelsen na msaidizi wake Jamhuru Kihwelo wakipongezana baada ya
mchezo kumalizika.
Mshambuliaji wa timu
ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys, Hussein Twaha akiwatoka
mabeki wa timu ya Congo Brazzaville katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za
Afrika kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Mchezo
huo ulifanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Serengeti Boys
imeshinda 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya
Srengeti Boys, Faridi Mussa (katikati) akiwania mpira huku beki wa Cpngo
Brazzaville, Tmouele Ngampio akijaribu kumzuia. Kulia ni Golipika wa Congo
Brazzaville, Ombandza Mpea akijaribu kuokoa hatario langoni
mwake.
Waamuzi wa mchezo huo
wakitoka baada ya kwisha kwa pambano hilo
Mshambuliaji wa
Serengeti Boys, Tumain Baraka akichuana na beki wa Congo Brazzaville, Okombi
Francis
Heka heka katika lango
la Congo Brazzaville
Wachezaji wa Serengeti
Boys, Hussein Twaha (shoto), Joseph Lubasha na Selemani Hamis Bofu
wakibadilioshana mawazo wakati wakitoka mapumziko
Selemani Hamis Bofu
akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Congo Brazzaville, Tmouele Mpira wa serengeti boys na Congo Brazaville umemalizika kwa Serengeti Boys kupata goli moja kwa bila , goli lililofungwa na Yahya abbas katika dakika ya 15, Vijana wa Jacob Michelsen wanahitaji sare yoyote katika mchezo wa pili utachezwa wiki mbili zijazo nchini CONGO BRAZAVILLE.
vikosi
vilikuwa:
Tanzania; Peter Manyika Peter, Miza Kriston Abdallah, Mohamed
Hussein Mohamed, Ismail Adam Gambo, Miraj Adam Suleiman, Mudathir Yahya Abbas,
Mohamed Salum Haroub, Joseph Kimwaga Lubasha/Dickson Isaac Ambundo, Hussein
Twaha Ibrahim, Suleiman Hamisi Bofu/Tumaini Baraka Mosha na Farid Mussa
Shah.
Kongo Brazzaville; Ombandza Mpea Joe, Tmouele Ngampio,
Mabiala
Gharlevy, Okimbi Francis,
Ondongo Boungena, Ibra Vinny/Issambey
Lonvreve, Binguila Handy,
Obassi Ngatsongo, Mohendiki Brel, Atoni
Mavoungou na Biassadila
Arei.
Post a Comment