Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA KWA UMMA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


TAARIFA KWA UMMA


UTARATIBU WA KUOMBA LESENI YA BIASHARA YA NYARA (TROPHY DEALERS LICENCE- TDL)
KWA MWAKA 2013.
Wizara ya Maliasili na Utalii inawajulisha wananchi ambao wangependa kufanya biashara ya nyara kuwasilisha maombi yao kwa Maafisa Wanyamapori wa Wilaya ambao watawapatia fomu za maombi.
Fomu za maombi zilizojazwa zinatakiwa kuwasilishwa kwa Maafisa Wanyamapori wa Wilaya husika ndani ya siku 14 tangu kuchapishwa tangazo hili. Yaani, mwisho wa kuwasilisha ni tarehe 26 Novemba 12012.
Biashara ya nyara ni moja ya matumizi ya wanyamapori yanayofanyika kwa madhumuni yafuatayo:
(i) Kuongeza mapato ya Serikali;
(ii) Kuongeza mapato ya wananchi;
(iii)Kuhamasisha wananchi katika kutambua umuhimu wa uhifadhi.
Daraja zitakazoruhusiwa kufanyiwa biashara kwa mwaka 2013 ni kama ifuatavyo:

Daraja
Maelezo
2-10
Mazao ya Wanyamapori
11
Wakala wa usafirishaji wa nyara kwa ujumla (clearing and forwarding)
12
Daraja la 12 ambalo linahusu biashara ya ndege hai. Ndege watakaoruhusiwa ni ndege aina ya “kingfishers, bee-eaters, rollers, larks, bulbuls, thrushes, starlings, weavers, waxbills, canaries, seed – eaters, and sunbirds”.
13
“live primates” yaani nyani mwekundu, nyani njano, tumbili, na kima (olive baboon, yellow baboon, vervet monkey and blue monkey).
15
Wanyama wanaotambaa (reptiles).
16
Wafanyabiashara wanaotaka kujihusisha na biashara ya wanyama aina ya “amphibians” kama walivyoainishwa kwenye Kanuni za Ukamataji Wanyamapori, 2010.
17
Bustani ya wanyamapori.
18
Mashamba ya ufugaji wa wanyamapori.
19
Vituo vya karantini (Quarantine station).
20
Ranchi za wanyamapori.
21
Shughuli nyingine inayohusiana na nyara tofauti na zilizoorodheshwa kwenye daraja 1-10 na 11-20.

Maombi ya leseni ya biashara ya nyara kwa madaraja hayo kwa mwaka 2013 yawasilishwe kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori baada ya kupitishwa na Afisa Wanyamapori wa Wilaya (DGO) husika ndani ya siku 15 toka tarehe ya mwisho yakutuma maombi.
Mwombaji anatakiwa kuwasilisha fomu ya maombi ya leseni pamoja na uthibitisho wa yafuatayo:-
1. Hati ya usajili wa jina la biashara (certificate of registration) au hati ya makubaliano ya biashara (Memorandum and Articles of Association) endapo mwombaji ni kampuni.
2. Hati ya utambulisho wa mlipa kodi (Tax payer Identification Number).
3. Uthibitisho kwamba ameajiri Wakamataji wenye uzoefu usiopungua miaka mitatu na angalau wenye mafunzo ya uhifadhi wa wanyamapori kutoka chuo kinachotambulika endapo mwombaji anatarajia kufanya biashara ya wanyamapori hai.
4. Uthibitisho wa upatikanaji wa masoko ya wanyamapori hai na mazao yatokanayo na wanyamapori.
5. Uthibitisho kwamba biashara ina leseni kutoka kwenye mamlaka husika.
6. Mpango wa biashara (Business plan) unaohusu biashara inayotarajiwa kufanywa na uthibitisho wa kuwa na mtaji.
7. Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi ya leseni (TZS 5,000.00) ambayo haitarudishwa (Non-refundable). Fedha hizo zilipwe kupitia Benki ya NMB akaunti Na. 2011100080 ya “Tanzania Wildlife Protection Fund”.
8. Mwombaji asiwe amewahi kupatikana na hatia ya kuvunja Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009.
9. Uthibitisho wa kuwa na eneo/zizi la kuhifadhi wanyamapori lenye sifa stahili pamoja na vifaa/vitendea kazi vingine vinavyohusiana na biashara husika.
10. Mwombaji awe amepata kiwango cha matumizi ya mgawo wa Wadudu (quota) wa mwaka uliopita kisichopungua asilimia kumi (10%) endapo mwombaji alifanya biashara mwaka uliopita.


G. Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
13 Novemba 2012
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top