Kiongozi wa Askari
magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na wenzake, kutoka mahakama ya hakimu mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa kwa kesi yao.
Sheikh Ponda Issa Ponda,
akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Novemba 1, 2012.
Kiongozi
huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu anayesikiliza kesi
dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe jijini Dar es
Salaam, ambapo waliharibu na kuiba mali mbali mbali zenye thamani ya shilingi
milioni 59, madai ambayo washtakiwa wote waliyakanusha.
Hakimu huyo
alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni
mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP),
hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba
moja.
Ulinzi katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi kutokea
katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV
Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa kutuliza
ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na askari kanzu
waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na mahakama hiyo kubwa jijini Dar es
Salaam.
Kikundi kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda, kilijaribu kuleta
rabsha, lakini polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani
ambapo pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye
waliondoka huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la
makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao
wakatawanyika.
Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo
taarifa kuwa wafuasi hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na
pia walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanya
maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe.
Kesi hiyo
imeahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena
Sheikh Ponda na pingu zake
mikononi, akirejeshwa rumande.
 |
| Wafuasi
wa Ponda, wanbaoshatakiwa pamoja naye, wakifunguliwa pingu
mahakamani |
 |
| Mshtakiwa
akiwa amebebwa na mwenzake baada ya kudondoka mahakamani na kupoteza
fahamu |
 |
| Askari wa
kutuliza ghasia magereza, akiwa ameshika lindo mbele ya mahakama ya hakimu mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba 1,
2012 |
 |
| Polisi wa
Mbwa nao walichukua nafasi yao |
 |
| Huiingii
mahakama ya Kisutu bila ya kukaguliwa na mashine za kugundua vitu vya asili ya
chuma hapo. |
 |
| Farasi wa
polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh Ponda, waliojikusanya nje ya uzio
wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Alhamisi Novemba 1,
2012 |
 |
| Polisi wa
Mbwa wakisubiri amri ndani ya gari lao nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es
Salaam, Novemba 1, 2012 |
 |
| Polisi wa
Mbwa akifanya doria kwenye barabara ya Bitbi Titi mbele ya jengo la mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam |
 |
| Askari Magereza wa kutuliza ghasia, aliyejihami kwa
silaha na vifaa vingine akiwa makini kulinda usalama |
on Thursday, November 1, 2012
Post a Comment