Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa hapo Bungeni mjinni Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Novemba 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
**************************
Amani na utulivu uliopo hapa nchini Tanzania utazidi kudumishwa daima ikibidi kwa njia yeyote na watanzania wawe na amni na kufanya kazi zao bila kuwa na wasiwasi wowote.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahakikishia watanzania leo wakati akijibu maswali ya wabunge mjini Dodoma katika kikao cha tatu la Bunge la Kumi kinachoendelea mjini Dodoma.
Pinda amesema kuwa kama kuna mtu anadhani kuwa kwa kuleta chokochoko yake ataondoa amani na utulivu uliopo hapa nchini Tanzania, basi mtu huyu anajisumbua na hayuko sahihi hata kidogo.
Amesema kuwa ni kweli kuna baadhi ya watu wengine wanajipatia kipato kwa kutaka kiuanzisha fujo za kidini, watu wa aina hiyo tunawajua kwa sura na majina yao. Waziri ameahidi kuwachuklia hatua kali za kisheria na kuwafikisha mahakamani.