KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi
*************
NA BASHIR NKOROMO, RUKWA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
amesema, CCM itamtosa bila kumuonea haya mwanachama yeyote atakayeomba
kuteuuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM huku akiwa kinara wa kutegemea
makundi kumwigiza katika nafasi hiyo.
Badala yake CCM itahakikisha mgombea
inayemsimamisha ni mwana CCM asiyeendekeza makundi, mwadilifu ambaye kila
akiteuliwa atakuwa hatiliwi shaka.
Kinana alisema hayo leo, wakati akijibu swali
la mmoja wa wana-CCM katika mkutano wa wana CCM shina la Isesa mkoani hapa,
akiwa katika ziara ya kujitambulisha yeye na sekretarieti mpya na kueleza
usimamizi na utekelezaji wa ilani ya Chama.
Mwana CCM huyo,Peter Lilata aliitaka kujua CCM
imejiandaa vipi kuhakikisha katika uchaguzi mkuu wa 2015, CCM inateua mgombea
ambaye atakubalika na wananchi wengi, na kutofanye kosa kuteua mgombea ambaye
hakubaliki kwa kuwa kufanya hivyo kutaisababishia usumbufu mkubwa CCM katika
kupata ushindi.
Mapema akizungumza baada ya kuzindua shina
hilo, ambapo alilichangia sh. 500,000 ili kujiimarisha, Kinana aliwataka
viongozi wa CCM kuonyesha mfano wa ujenzi wa Chama kwa kutembelea ngazi za
mashina na matawi.
"Kuanzia sasa tutawapima viongozi wetu kwa
namna wanavyokuwa wepesi kutembelea mashina na matawi ya CCM , kwa sababu
utaratibu huu ndiyo pekee utakaokiimarisha Chama, na si vinginevyo", Kalisema
Kinana na kuongeza;
"Kutokana na kutambua hilo na kwa kuwa ni
maelekezo yaliyotokana na maazimio kwenye Mkutano wetu Mkuu uliomalizika hivi
karibuni mjini Dodoma, ndiyo sababu baada ya kupatiwa wadhifa huu (Ukatibu Mkuu
wa CCM) mimi na wenzangu tumeanza ziara hii, na kila ninapofika lazima
nitembelee mashina na matawi ili kuwa mfano kwa viongozi wengine".
Kinana alisema, litakuwa jambo la ajabu sana
ikiwa yeye kwa nafasi yake ya Ukatibu Mkuu anatembelea mashina na matawi,
viongozi wa ngazi zingine wasifanye hivyo.
Akizungumzia suala la rushwa,izengwe katika
uchaguzi, Kinana aliwataka wana-CCM kuhakikisha katika kila chaguzi wanahangaika
kuunga mkono wagombea ambao ni watendaji wazuri na wenye maadili safi badala ya
kukumbatia wanaowapa rushwa.
"Lazima mjue kwamba, mnapoamua kumchagua
mgombea anayewapa rushwa, mnafanya kosa kubwa sana kwenu, maana akishapita
anakuwa kiongozi wa kutetea maslahi yake na siyo yenu", alisema
Kinana.
Alisema, pamoja na kuwepo viongozi wanaotoa
rushwa kutafuta uongozi, lakini, wananchi nao wamekuwa chanzo cha kukomaza
rushwa kwa sababu mwanachama mwenzao anapojitokeza kuomba uongozi, huwa wa
kwanza 'kutengeneza'mazingira ya kumtaka atoe rushwa huku wakionyesha kwamba
hawezi kupenya asipofanya hivyo.
Kinana alaiwataka wana-CCm kuacha kutungiana
fitina, mizengwe na kuachana na makundi kabisa kila baada ya chaguzi kwa sababu
mambo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha mshikamano na umoja ndani
ya chama ambao ndiyo siri ya ushindi.
Kinana ambaye katika ziara hiyo anafuatana na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnuauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni
Mohamed Seif Khatib na baadhi ya mawaziri, aliwasili Rukwa leo akitokea mkoani
Mtwara ambako alifanya mikutano kadhaa na kutembelea mashina na matawi ya
CCM.



Post a Comment