Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe
mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda leo mchana kwa ajili ya
kushiriki katika shughuli ya uzinduzi rasmi wa mkoa huo utakaofanyika siku ya
jumapili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, mkoa huo ukizunduliwa rasmi
kwa ving'ola na Mh Dkt. Gharib Bilal Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania anayetarajiwa kuwasili kesho mjini Mpanda tayari kwa ajili ya uzinduzi
huo
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda viongozi mbalimbali wa CCM baada ya kuwasili mkoani Katavi
leo mchana katikati ni Waziri wa Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu na kulia ni Mkuu wa
mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rtengwe.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema)
mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe kwa
ajili ya kukagua vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpanda mara baada
ya kuwasili, kushoto ni mke wake mama Tunu Pinda.
Mke wa
Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda kushoto akifurahia jambo na Dkt. Mary Nagu waziri wa
Uwezehaji Ofisi ya Waziri Mkuu wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa
mpanda leo mchana.
Mh.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akuwapungia mkono wakazi wa mjini Mpanda waliofika
uwanja wa ndege kumlaki , kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab
Rutengwe.
Kikundi
cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa
Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema) wakati wa mapokezi ya waziri kuu Mizengo Pinda
mjini Mpanda, Mh. Rajab Rutengwe anatoa kauli mbiu yake kuwa "SIASA NI
MAENDELEO".
Mkuu wa mkoa
wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe akimsiliza Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi
kamanda Dhahiri Kidavashari wakati akimpa maelezo ya utaratibu wa mapokezi ya
mgeni huyo, kulia anayesikiliza kwa makini ni Afisa Habari wa mkoa wa Rukwa Bw.
Hamza Temba
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Mkoa
wa Rukwa ili kupata maelezo kadhaa katika maonyesho hayo kulia ni Mkuu wa mkoa
wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu
Pinda.




Post a Comment