Warembo mbalimbali wanaoishi
Ulaya na walioshinda katika mashindano ya Miss East Africa huko Ulaya pia
watashiriki katika mashindano ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika tarehe
07 December katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam warembo
hao ni:
1. MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia
Ikwene (24)
2.MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg
Marcos (21)
3.MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona
Ruboneka (24)
Fainali za mashindano ya Miss
East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi,
Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu
yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani
kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza
utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na
kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa
yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es
salaam.
MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg
Marcos (21)
Post a Comment