Meneja Huduma kwa
wateja wa benki ya NMB Tawi la Bank House Steven Chavala (mwenye Suti Nyeusi)
akibonyeza kitufe kuwapata washindi wa promosheni ya Ki-College zaidi na NMB.
Kutoka (kushoto) ni Meneja Amana wa NMB, Boma Raballa, Meneja Masoko wa NMB,
Shilla Senkoro na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha ya Taifa, Humud
Abdulhussein na Meneja bidhaa wa selcom, Julio Batalio.
Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha
zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua
Meneja wa
Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah akibonyeza kitufe cha kompyuta kuwatafuta washindi
wa promosheni hiyo.
Meneja wa
Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah (wa pili kulia) akiangalia
namna washindi wa promosheni ya Ki-College Zaidi na NMB wanavyopatikana wakati
wa droo ya kwanza iliyochezeshwa Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam
jana. Kulia ni Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhussein. Kushoto
ni Meneja wa Amana, Boma Raballa na Meneja Masoko, Shilla
Senkoro
..........................
Octoba 1, 2012
NMB ilizindua promosheni ya Ki-COLLEGE zaidi na NMB inayowawezesha wanafunzi
wenye akaunti ya NMB Student Account kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na
kujishindia zawadi mbalimbali kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash
disk, fulana za NMB, taa inayotumia mionzi ya jua. Hivyo basi, wanafunzi
waliofungua NMB Student Account, walioweka amana katika akaunti
zao au kujiungana NMB mobile wameweza kuingia kwenye droo na wamepata nafasi ya
kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na
NMB.
Katika droo ya kwanza ya Ki COLLEGE zaidi na NMB iliyochezeshwa
tarehe 12 Novemba, 2012, jumla ya washindi 66 walijishindia zawadi mbalimbali
kama ifuatavyo; Ipad 2, Samsung Galaxy 2, Amana
maradufu 2, taa inayotumia mionzi ya jua na jezi za timu ya Taifa
30.
Pamoja na kampeni hii, wanafunzi walioshinda na watakao fungua NMB
Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB Student Account kama:
Kufungua akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB ATM kadi),kujiunga na huduma
ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya
NMB bure, kuchukua fedha hadi Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata
huduma kupitia matawi zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi
nzima.
Ili uweze kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi
kwenye promosheni ya Ki COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB Student Account, weka
amana katika akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile .Ikiwa hujatumia
akaunti yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe ushiriki katika
promosheni hii ya ki-COLLEGE zaidi na NMB inayoendelea hadi Desemba 31, 2012.
Post a Comment