![]() |
| Yanga wamemaliza kileleni |
Na Mahmoud
Zubeiry
MZUNGUKO wa
kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, rasmi umemalizika jana ukiacha
mechi mbili za viporo za Tanzania Prisons, dhidi ya Mgambo JKT na Ruvu
Shooting.
Prisons
walipata ajali wakiwa njiani kuelekea Tanga kwa ajili ya mechi yao na Mgambo
JKT, hivyo mechi hiyo na ile iliyofuata dhidi ya Ruvu Shooting zikaahirishwa na
kupangiwa tarehe nyingine, ili kuwapa wachezaji wake nafasi ya kupona
majeruhi.
Mzunguko wa
kwanza umemalizika na matokeo yamekuwa tofauti na mwelekeo wa ligi hiyo katika
mzunguko huo, hadi katikati yake.
Yanga SC,
ambayo haikutarajiwa kushika hata nafasi ya pili, ndiyo imemaliza kileleni kwa
pointi zake 29, baada ya mechi hizo 13, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 24 na
Simba SC yenye pointi 23.
Presha
ilikuwa upande wa mashabiki wa Yanga ndani ya mechi tano za mzunguko wa kwanza,
kutokana na kuanza vibaya, kiasi cha kufikia kumfukuza kocha wake aliyewapa
ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Mbelgiji, Tom
Saintfiet.
Saintfiet
alifukuzwa baada ya mechi mbili za Ligi Kuu, akitoa sare na Prisons mjini Mbeya
na kufungwa mabao 3-0 na Mtibwa Sugar mjini
Morogoro.
Azam nayo
ilianza vema ikiwa nyuma ya Simba SC, lakini ilifukuza kocha wake Mserbia Boris
Bunjak baada ya kufungwa mabao 3-1 na Wekundu hao wa Msimbazi.
Naam,
Tanzania mechi moja au mbili za kufungwa zinatosha kumfukuzisha kocha na watu
sasa wanasubiri hatua itakayochukuliwa na Simba dhidi ya kocha wake, Mserbia
pia, Profesa Milovan Cirkovick baada ya klabu hiyo kufungwa mechi mbili
mfululizo, 2-0 na Mtibwa Sugar na 1-0 na Toto.
Tayari kundi
la Friends Of Simba ambalo linasaidia sana uendeshwaji wa klabu hiyo
limeripotiwa kushinikiza Milovan afukuzwe na Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj
Ismail Aden Rage amesema Ijumaa wiki hii atachukua maamuzi magumu.
Tusubiri.
Lakini
tumeshuhudia timu mpya iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ambayo imeleta changamoto
mpya, JKT Mgambo pamoja na kuimarika kwa Coastal Union, Kagera Sugar na Mtibwa
Sugar, ambazo zinatoa upinzani katika ligi hiyo hata kwa
vigogo.
Kwa kiasi
kikubwa msimu huu tuna ligi tofauti na ya msimu uliopita na kama timu zitafanya
maandalizi mazuri kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili, ni matarajio ya wengi
Ligi Kuu itaisha vizuri zaidi.
![]() |
| Yanga SC 2012 |
YANGA
SC:
Wamemaliza
mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu, wakiwa na pionti zao 26, baada
ya kucheza mechi 13, kufungwa mbili dhidi ya Mtibwa Sugar 3-0 na Kagera Sugar
1-0, zote ugenini, kutoa sare mbili 1-1 dhidi ya Simba SC na 0-0 dhidi ya
Prisons.
Yanga ambayo
msimu uliopita ilishika nafasi ya tatu Ligi Kuu, ilipanda kileleni Novemba 4,
baada ya kuifunga Azam FC mabao 2-0 na kuwashusha mabingwa watetezi, walioongoza
ligi hiyo tangu mwanzoni.
Katikati ya
mzunguko wa kwanza, Yanga ilifikia kuzidiwa pointi saba na Simba lakini Oktoba
31, ikafanikiwa kuwafikia Wekundu hao wa Msimbazi, siku hiyo wao wakiifunga
Mgambo JKT 3-0 Dar es Salaam na wapinzani wao wakilazimishwa sare ya bila
kufungana na Polisi Morogoro.
P W D L GF GA GD
Pts
1 Yanga
SC 13 9 2 2 25 10 15
29
![]() |
| Azam FC 2012 |
AZAM
FC:
Imemaliza
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya pili, kwa pointi zake 24,
ikiwazidi pointi moja tu mabingwa watetezi, Simba SC. Azam walikuwa na mwelekeo
wa kumaliza katika nafasi nzuri zaidi kama si kufungwa mechi mbili mfululizo za
mzunguko wa kwanza, dhidi ya Yanga 2-0 na Mgambo JKT
2-1.
Azam ilianza
vema tu ligi hiyo, ikiwa nyuma ya Simba tangu mwanzo hadi Oktoba 31,
ilipoenguliwa na Yanga katika nafasi ya pili. Ikielekea kwenye mechi yake ya
mwisho dhidi ya Mgambo, Azam ilifukuza wachezaji wake wanne, Deo Munishi ‘Dida’,
Erasto Nyoni, Said Mourad na Aggrey Morris kwa madai walipokea hongo waifungishe
timu hiyo dhidi ya Simba na wanadai wana ushahidi hadi wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Dhahiri kuondolewa kwa wachezaji hao tegemeo
kikosini kulichangia matokeo ya kufungwa na Mgambo katika mechi ya mwisho.
P W D L GF GA GD
Pts
2 Azam
FC 13 7 3 3 17 11
6 24
KOCHA:
Stewart Hall (Uingereza)
![]() |
| Simba SC 2012 |
SIMBA
SC:
Mabingwa hao
watetezi, waliianza Ligi Kuu vema wakionyesha dalili zote za kutetea ubingwa wao
kwa kufanikiwa kuwa kileleni hadi mwishoni mwa mzunguko huo, kabla ya mambo
kugeuka ghafla.
Zilianza
sare kwanza, 1-1 na Yanga, 0-0 na Coastal Union, 2-2 na Kagera Sugar na baadaye
0-0 na Mgambo, 0-0 na Polisi Morogoro kabla ya kufungwa mechi ya kwanza msimu
huu, mbele ya Mtibwa Sugar na kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kipigo cha 1-0
kutoka kwa Toto Africans.
Matokeo haya
kwa kiasi kikubwa yameivuruga Simba SC na inasemekana Makamu Mwenyekiti wa klabu
hiyo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ anafikiria kujiuzulu na baada ya kufungwa na
Mtibwa Sugar, hakujihusisha na chochote juu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya
Toto, wakati huo Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage yuko bize na shughuli
za kisiasa Dodoma. Rage anasema amekwishawajua wanaosababisha matokeo mabaya
Simba na Ijumaa atatangaza maamuzi magumu.
P
W D L GF GA GD Pts
3 Simba
SC 13 6 5 2 20 11
9 23
KOCHA:
Milovan Cirkovick (Serbia)
![]() |
| Mtibwa Sugar 2012 |
MTIBWA
SUGAR:
Ilianza
vizuri, katikati ikavurunda na mwishoni mwa mzunguko wa kwanza ikazinduka tena
hatimaye imemaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi
Kuu.
Inaonekana
Mtibwa Sugar inaanza kurejesha makali yake iliyoingia nayo katika soka ya
Tanzania miaka ya 1990 hadi wakafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara mbili
mfululizo 1999 na 2000, wakiweka rekodi ya kuwa timu pekee nje ya Simba na Yanga
kutetea taji hilo.
Hiyo si kwa
sababu tu ipo nyuma ya Yanga, Azam na Simba, bali msimu huu imefanikiwa
kuvifunga vigogo vyote vya soka nchini, Simba na Yanga.
P W D L GF GA GD
Pts
4
Mtibwa Sugar 13 6 4 3 18 12 6
22
KOCHA:
Mecky Mexime (Mzalendo)
![]() |
| Coastal Union 2012 |
COASTAL
UNION:
Wana
Mangushi wamerudi tena kwenye makali yao yaliyowafanya wakawa mabingwa wa ligi
hiyo mwaka 1988, kwani hadi sasa wameonyesha upinzani wa kutosha kwenye Ligi
Kuu. Wagosi hao wa Kaya wamemaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi
Kuu kwa pointi zao 22 sawa na Mtibwa walio nafasi ya nne, lakini wanazidiwa
wastani tu wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hata hivyo,
Coastal walianza Ligi Kuu kwa kusuasua kiasi cha kufikia kuwafukuza makocha wake
wa awali waliosajili na kuandaa timu kwa ajili ya ligi hiyo, Juma Mgunda na
Habib Kondo ambao nafasi zao zilichukuliwa na Hemed Morcco na Ally
Kiddy.
P W D L GF GA GD
Pts
5
Coastal Union 13 6 4 3 16 14 2
22
KOCHA:
Hemed Morocco (Zanzibar)
![]() |
| Kagera Sugar 2012 |
KAGERA
SUGAR:
Kagera Sugar
wamemaliza katika nafasi ya sita wakiwa na pointi 21 na wangeweza kumaliza juu
ya hapo, kama wangeutumia vizuri mchezo wao wa mwisho kwenye Uwanja wa nyumbani
dhidi ya vibonde Polisi Morogoro.
Wakipewa
nafasi kubwa ya kushinda, katika mastaajabu ya wengi, Kagera wakalazimishwa sare
ya bila kufungana na Maafande hao wa Morogoro kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba,
hivyo kuwapa nafasi Coastal na Mtibwa kuendelea kuwa juu
yao.
Kagera
inajivunia kutofungwa na vigogo wa soka nchini, kwani waliifunga Yanga 1-0 na
wakatoa sare ya 2-2 na Simba na Dar es Salaam.
P W D L GF GA GD
Pts
6
Kagera Sugar 13 5 6 2 15 10 5
21
KOCHA:
Abdallah Athumani Seif ‘Kibadeni’
(Mzalendo)
![]() |
| Ruvu Shooting 2012 |
RUVU
SHOOTING:
Katika timu
zote za majeshi kwenye ligi hiyo, Ruvu Shooting ndio inaonekana kuwa imara zaidi
na ndiyo maana ipo katika nafasi nzuri zaidi, ikiwa imebakiza mechi moja ya
kiporo dhidi ya Prisons kumaliza mechi zake za mzunguko wa
kwanza.
Ruvu ipo
katikati ya msimamo wa ligi, nafasi ya saba kwa pointi zake 17 na inaweza
kumaliza na pointi 20 iwapo itaifunga Prisons, lakini itaendelea kubaki kwenye
nafasi hiyo hiyo, kwani Kagera Sugar waliopo juu ya wana pointi
21.
Timu hii
inayotumia Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani ni moja kati ya timu
zilizoonyesha kandanda safi ya kuvutia, tena ikiundwa na wachezaji wengi
chipukizi, kama Seif Abdallah anayegombea kiatu cha dhahabu.
P W D L GF GA GD
Pts
7 Ruvu
Shooting 12 5 2 5 17 17 0
17
KOCHA:
Charles Boniface Mkwasa (Mzalendo)
![]() |
| JKT Ruvu 2012 |
JKT
RUVU:
Imeshuhudiwa
katika msimu mwingine, timu hii inazidi kupoteza makali yake, baada ya kumaliza
katika nafasi ya nane mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu.
Siyo JKT ile
ambayo ilikuwa tishio kwa vigogo, Simba na Yanga bali hii ya sasa ni ‘urojo’ na
hali hii inatokea huku ikiwa inaundwa karibu na asilimia kubwa ya wachezaji wake
wale wale, walioifanya iwe tishio misimu michache iliyopita, tena wakiwa chini
ya kocha yule yule, kiungo wa zamani wa Yanga, Charles
Killinda.
P W D L GF GA GD
Pts
8 JKT
Ruvu 13 4 3 6 13 20 -7
15
KOCHA:
Charles Kilinda (Mzalendo)
![]() |
| TZ Prisons 2012 |
TZ
PRISONS:
Imerejea
Ligi Kuu msimu huu na hadi sasa unaweza kusema inapambana kuhakikisha inabaki
kwenye ligi hiyo msimu ujao. Prisons wana mechi mbili za viporo dhidi ya Mgambo
JKT na Ruvu Shooting ambazo zote watacheza ugenini, lakini hadi sasa inashika
nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Timu hiyo
iliahirishiwa mechi zake baada ya kupata ajali, ikiwa inaelekea Tanga kumenyana
na Mgambo na wachezaji wake sita wakaumia. Inaweza kupanda juu kiidogo iwapo
itashinda mechi zake mbili zilizobaki.
P W D L GF GA GD
Pts
9
Prisons 11 3 5 3 8 9 -1
14
KOCHA:
Jumanne Charles (Mzalendo)
![]() |
| JKT Oljoro 2012 |
JKT
OLJORO:
Haina makali
yake iliyoingia nayo kwenye Ligi Kuu msimu uliopita yaliyowafanya wamalize
mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni. Msimu huu JKT Oljoro imemaliza katika nafasi
ya 10 kwa pointi zake 24 na huwezi kusita kusema ipo kwenye hatari ya kushuka
daraja hadi sasa.
Ina pointi
14, sawa na Toto Africans iliyo nafasi ya 11 na inabebwa juu kwa wastani wa bao
moja tu katika mabao ya kufunga na kufungwa, huku ikiwa inaizidi kwa pointi
mbili tu Africans Lyon iliyo nafasi ya 12- JKT Oljoro hakika imemaliza mzunguko
wa kwanza katika eneo baya.
P W D L GF GA GD
Pts
10 JKT
Oljoro 13 3 5 5 13 16 -3
14
KOCHA:
Mbwana Makatta (Mzalendo)
![]() |
| Mgambo JKT 2012 |
MGAMBO
JKT:
Ligi Kuu ya
Bara imepokea timu mpya tushio ambayo imeongeza ladha katika ligi hiyo. Hiyo si
nyingine zaidi ya JKT Mgambo ua Handeni, Tanga inayotumia Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga pamoja na Coastal Union. Ikiwa na mechi moja ya kiporo mkononi dhidi ya
Prisons, Mgambo ipo nafasi ya 11 kwa pointi zake 14 na kama ikifanikiwa kushinda
mchezo huo, inaweza kupanda hadi nafasi ya saba, itategemea pia na matokeo ya
mchezo mwingine wa kiporo kati ya Ruvu Shooting na Prisons. Mgambo walianza kwa
kusuasua na watu wakaitabiria itashuka daraja, ila ilipokuja kuzinduka mwishoni
mwa msimu, watu wamebadilisha kauli zao.
P W D L GF GA GD
Pts
11 Mgambo
JKT 12 4 2 6 9 13 -4
14
KOCHA:
Mohamed Kampira (Mzalendo)
![]() |
| Toto Africans 2012 |
TOTO
AFRICANS:
Wana
Kishamapanda bado wapo katika wakati mgumu, kwani wamemaliza Ligi Kuu wakiwa
katika nafasi ya 12, ambayo ni ndani ya nafasi tatu za kushuka
Daraja.
Washukuru
sana ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC kwenye mchezo wao wa mwisho wa
mzunguko wa kwanza, kwani umewainua kidogo, vinginevyo wangemaliza ligi hiyo
vibaya zaidi.
Lakini hii
ni timu ambayo inacheza kwa ushindani zaidi inapokutana na timu tishio, ila kwa
timu ambao zinaonekana si tishio, Toto hufanya vibaya. Bila shaka kuna kudharau
mechi, ambako ndiko kunawaponza na kama watabadilika mzunguko wa pili, wanaweza
kmufanya vizuri na kubaki Ligi Kuu.
P W D L GF GA GD
Pts
12 Toto
Africans 13 2 6 5 10 15 -5
12
KOCHA: John
Tegete (Mzalendo)
![]() |
| African Lyon 2012 |
AFRICAN
LYON:
Hali bado ni
tete African Lyon, ikiwa imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu katika nafasi
ya 13 kwa pointi zalke tisa. Licha ya kunolewa na kocha Muargentina, Pablo
Ignacio Velez, lakini Lyon wamekuwa vibonde tu hadi
sasa.
Mmiliki wa
timu hiyo, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ amesema kwamba ametenga dau la dola za
Kimarekani 200,000 kwa ajili ya kufanya usajili dirisha dogo ili kuimarisha
kikosi na miongoni mwa wachezaji aliowalenga ni Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa
wa Simba na Mbuyu Twite wa Yanga. Amesema kwa Twite atatoa dola 100,000, Ngassa
dola 40,000 na Okwi dola 60,000. Tusubiri, ila hadi sasa hali tete
Lyon.
P W D L GF GA GD
Pts
13 African
Lyon 13 2 3 8 9 20 -11
9
KOCHA:
Pablo Ignacio Velez (Argentina)
![]() |
| Polisi Morogoro 2012 |
POLISI
MOROGORO:
Imerejea
Ligi Kuu msimu huu, lakini haitakuwa ajabu mwishoni mwa msimu ikarudi tena
kucheza Ligi Daraja la kwanza. Timu ya Morogoro, imemaliza mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu, ikiwa inashika mkia. Polisi haijashinda mechi hata moja zaidi ya kutoa
sare nne na kufungwa mechi nyingine tisa.
Sijui
maajabu gani yatokee, msimu ujao tuendelee kuwa na timu ya Morogoro, kwani
kulingana na ushindani wa Ligi Kuu msimu huu, hakuna dalili za Polisi
kupona.
P W D L GF GA GD
Pts
14 Polisi
Morogoro 13 0 4 9 4 16 -12
4
KOCHA: John
Simkoko (Mzalendo)

















Post a Comment