Kiongozi wa kanisa Katoliki
duniani Baba Mtakatifu Benedict wa 16.
Kiongozi wa kanisa
Katoliki duniani Baba Mtakatifu Benedict wa 16 amejiunga na mtandao wa kijamii
wa Twitter.
Baba Mtakatifu
alifungua ukurasa huo kwa lugha ya Kiingereza ambao tayari umekwisha wavutia
watu 92,000.
Idadi hii
inatarajiwa kuongezeka mara kiongozi huyo mzaliwa wa Ujerumani atakapoandika
kitu kwenye ukurasa huo.
Bado hajasema
chochote hadi sasa tangu kuufungua.
Uongozi wa Vatican
umesema kuwa ataanza kuutumia rasmi tarehe 12 mwezi
huu.
Post a Comment