Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KUMEKUCHA CCM


* MANGULA AANZA KUWAHOJI WALE WOTE WALIOTUHUMIWA KWA RUSHWA
* AHADI YAKE YA KUISAFISHA RUSHWA CCM AMEANZA KUITEKELEZA

WAGOMBEA wanaodaiwa kutumia rushwa kushinda uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wako matumbo moto baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula kuanza kuwaita na kuwahoji, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Mbali na wagombea wanaodaiwa kushinda kwa rushwa, Mangula pia anawahoji baadhi ya wagombea walioshindwa na waliowasilisha malalamiko kupinga ushindi wa wenzao.
Habari kutoka ndani ya CCM, zilisema Mangula ambaye amepania kuwachukulia hatua ndani ya miezi sita walioshinda kwa rushwa, ameanza kuwaita na kuwahoji.
Mangula ambaye amepata kuwa Katibu Mkuu wa CCM taifa wakati Mwenyekiti wake wakati huo akiwa Rais Benjamin Mkapa, amekuwa akiwaita watuhumiwa hao na kukutana nao mjini Dodoma ambako ameweka kituo chake cha kazi.
Majina ya waliowekwa kitimoto yamehifadhiwa kwa sasa, lakini walioitwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa taifa wa moja ya jumuiya za CCM ambao uchaguzi wao ulielezwa kutawaliwa na vitendo vya rushwa.
Jumuiya za CCM ni pamoja na Umoja wa Vijana (UVCCM), Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazee ambako uchaguzi wao uligubikwa na matukio ya rushwa ya waziwazi.
Tayari baadhi ya waliokuwa wagombea wa jumuiya hizo, wameandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM, kupinga ushindi wa wagombea na kutaka urudiwe upya.
Kwa mujibu wa habari hizo, Mangula anaendelea kuwaita wote waliolalamikiwa na walalamikaji kwa nyakati tofauti ili kupata maelezo yao na ushahidi kabla ya vikao vya juu kupitia rufaa hizo na kuzitolea maamuzi.
Tangu kumalizika kwa uchaguzi ndani ya CCM, kumekuwa na malalamiko mengi ya kupinga ushindi wa baadhi ya wagombea, huku Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akiwa mtu wa kwanza kulalamika kuwa ameangushwa kwa rushwa ya mtandao. Sumaye aliangushwa na Dk. Mary Nagu.
Mangula ambaye amejigamba kuwavua ushindi baadhi ya vigogo CCM, akiwemo mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji, alisema katika kushughulikia suala hilo, hawatasubiri uamuzi wa mahakama kwani ushahidi wa mazingira unatosha kabisa kuwaengua wanaodaiwa kushinda kwa rushwa.
Hata hivyo, wadadisi wa mambo ya siasa nchini wanasubiri kwa hamu kuona kama kweli Mangula na sekretarieti mpya, chini ya Abdulrahman Kinana, wana ubavu wa kufanya maamuzi magumu ya kutengua ushindi wa vigogo wanaodaiwa kushinda uchaguzi kwa rushwa.

Chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top