|
DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa
Mbeya,Paul Kisabi (32), anayetuhumiwa kwa kupokea rushwa ya sh
100,000 |
|
Hapa daktari huyo akiwa na maafisa wa Takukulu wakiingia
mahakamani |
|
Hapa Dr huyo akiongea na wakili
wake
DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa
Mbeya,Paul Kisabi (32), amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya,
akikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi
100,000 kutoka kwa mgonjwa aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata
ajali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na
Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa
tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea
mtego.
Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani majira ya saa 3:45 na
kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya,
Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali
kwa wananchi.
Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka
uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod Mafwele.
Waendesha mashitaka
hao walidai kuwa Disemba 19 majira ya asubuhi akiwa katika sehemu yake ya kazi
katika kitengo cha upasuaji, mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la kushawishi
rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown, aliyefika hapo kwa
lengo la kupatiwa matibabu.
Walisema katika kosa la pili, siku hiyo majira ya
saa nane mchana akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la Victoria iliyopo
Jijini hapa, mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo ya shilingi
100,000, huku akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria.
Walisema
kuwa kwa mujibu wa sheria za taasisi hiyo, makosa yote yaliyotendwa na
mshitakiwa yanaangukia kwenye kifungu cha 15 ibara ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia
rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo,
Wakili wa mshtakiwa huyo, Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama impe dhamana mteja
wake akidai kuwa makosa yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Kishenyi
alikubaliana na maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote yanayomkabili
mshtakiwa yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi.
Alimtaka mshtakiwa huyo
kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani
ya Sh,500,000, na kwamba awe na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa
serikali ya mtaa .
Hata hivyo mahakama ililazimika kuahirishwa kwa muda wa
dakika 20 ili kutoa nafasi kwa mdhamini wa mshitakiwa kuleta barua hiyo baada ya
kudai kuwa alikuwa ameisahau kwenye gari lililokuwa nje ya jingo la
mahakama.
Baada ya kupokea ombi hilo hakimu Kishenyi aliwahoji waendesha
mashitaka kama wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja walikubali kwa maelezo kuwa
dhamana ni haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo hawakuwa na
pingamizi.
Mshitakiwa aliweza kutimiza masharti ya dhamana hiyo na hivyo
kuachiwa huru hadi januari 7 mwaka 20013 ambapo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa
katika mahakama hiyo.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za mahama hiyo, mshitakiwa huyo
Daktari Kisabi ni mmoja wa mashahidi wa kesi nyingine inayoendelea mahakamani
hapo ya mtoto Anethi anayedaiwa kuchomwa moto katika mkono wake, kufungiwa ndani
na kulazimishwa kula kinyesi chake na Shangazi yake.
59
Habari na moses picha Mbeya
yetu |
on Thursday, December 20, 2012
Post a Comment