Rais Mwai Kibaki wa Kenya leo analihutubia bunge la nchi hiyo huku wananchi wakitarajia kusikia mengi kutokana na hali halisi ilivyo katika nchi hiyo kwa sasa.
Kuanzia upande wa misimamo ya kisiasa, maandalizi ya uchaguzi, suala la baadhi ya watu wake kushutumiwa kuchochea vurugu za mara baada ya uchaguzi na kushitakiwa katika mahakama ya ICC na kuyumba kwa hali ya usalama kufuatia kuwepo kwa milipuko ya mashambulizi ya mara kwa mara yanayodaiwa kufanywa na al-Shabaab.