KUTOKANA na Klabu ya
Simba kukabiliwa na ukata wa fedha, inaelekea kushindwa kumbakisha mshambuliaji
wake wa kimataifa, Mganda Emmanuel Okwi ambaye anataka dau la dola 40,000 za
Marekani kabla ya kusaini mkataba mpya, imefahamika.
Kwa mujibu wa habari
kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi zinasema tayari
Simba wameanza mazungumzo na Azam kwa lengo la kumuuza huko kwa kiasi cha fedha
watakachoafikiana.
Chanzo hicho kimedokeza
kuwa hatua ya kutaka kumuuza Okwi kwa Azam ni kutokana na Simba kutokuwa na
fedha za kumpa ili aweze kubaki katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza Ligi
ya Mabingwa Afrika mapema mwakani.
“Kwa kifupi Okwi ametaka
kiasi hicho cha fedha, kinyume na hapo hawezi kuongeza mkataba wa Simba katika
mzunguko wa pili na michuano ya kimataifa,” alisema kiongozi mmoja wa timu hiyo
ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Aliongeza kwamba kwa
sasa wanaelekeza nguvu zao kwa ajili ya kumuuza nyota huyo ili wapate fedha kwa
ajili ya usajili wa nyota wengine na kuwaongezea mikataba baadhi yao waliopo kweye kikosi
cha timu hiyo.
Alisema tayari wameanza
mazungumzo na Azam ya kumuuza Okwi na kudokeza kuwa mazungumzo ya awali
yamekwenda vizuri kwani sasa wanasubiri ofa watakayoitoa wao Simba
kuona kama wataimudu au
la.
Juhudi za kutaka kumuuza
Okwi zinakuja huku nyota huyo mahiri akibakisha miezi mitatu kwenye mkataba wake
wa kuitumikia timu hiyo inayopigana kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya
Bara.
Mkakati wa Simba kumuuza
nyota huyo umechukua kasi huku kukiwa na habari kuwa baadhi ya timu za Afrika na
Ulaya zimeonesha nia ya kumtaka nyota huyo mahiri kwa upachikaji mabao,
aliyeisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu
uliopita.
Okwi kwa sasa yupo
nchini
Post a Comment