WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Hawa Ghasia ameziagiza Halmashauri na Jiji la Dar es Salam kujadiliana na kupata
sheria nakanuni zitakazo ainisha utendaji kazi
wao.
Kauli hiyo ilitoa jijini
jana, na waziri huyo, wakati akifungua mkutano wa wabunge na madiwani, wa mkoa
huo, kwa ajili ya majadiliano, kuhusu mustakabali wa jiji
hilo.
Ghasia alisema kutokana na
mkanganyiko wa kazi za Mamlaka ya Jiji na zile za Halmashauri kutoeleweka,
mnapaswa kujadiliana hususan kuboresha sheria na kanuni zake ili kuimarisha
mahusiano, kupata sheria na kanuni zitakazo tambulisha mipaka ya mamlaka hizo
mbili kiutendaji.
Akizungumzia mradi wa
Mabasi ya endayo haraka (DART), alisema lengo la mradi huo, ni kuwa na usafiri
bora wa Umma wenye gharama nafuu, unaotumia mabasi
makubwa.
Ghasia alisema dhima ya
Mradi huo ni kutoa huduma bora na nafuu jijini na kuleta ukuaji wa uchumi
endelevu kwa wananchi na kuwa kichocheo baina ya Serikali na Sekta binafsi
katika nyanja ya usafirishaji wa umma jijini.
Mwenyekiti wa Kamati ya
DART, Dk Didas Masaburi ambaye pia ni Meya wa Jiji hilo, alisema wanatarajia
kukihamishia Mbezi Luis kituo cha mabasi yaendayo mokoani na nje ya nchi ifikapo
Januri 15, 2013 ili kupisha mradi huo wa DART.
Alisema kwa kuwa mradi huo
ni wa wananchi, hivyo kuanzia sasa ushiriki wa madiwani na wenyeviti utapewa
kipaumbele lengo likiwa ni kuwafikisha wananchi elimu kuhusu umuhimu wa mradi
huo katika jamii.
Naye Diwani wa Kata ya
Saranga (Chadema), Efraim Kinyafu alisema wakati ujenzi huo, bado hakuna juhudi
za makusudi za kupanua barabara ili kuepuka foleni katika eneo la kimara hadi
kituo kipya cha Mabasi Mbezi.
Mkutano umependekeza
maazimio tisa yakiwemo ya, mkutano kati ya Meya wa Jiji na madiwani wa
halmashauri kufanyika mara mbili kwa mwaka, kuundwa kamati itakayosimamia
uandaaji sheria na kanuni zitakazo ongoza mamlaka hizo na mengineyo ambayo
yatajadiliwa katika mkutano utakaofanyika hivi karibuni.
Akifunga Mkifunga Mkutano
huo, Naibu Katibu Mku (Tamisemi), Jumanne Mgini, alisema viongozi hao wanapaswa
kutambua kuwa suala la maendeleo yamo mikononi mwao, hivyo ni bora kila
wanapojadili maendeleo ya jiji hilo wanafikisha ujumbe sasa hii kwa wananchi
siyo vinginevyo.
Alisema suala la kuendeleza
jiji hilo ni lao wenyewe hivyo wawe tayari kupokea machungu yatakayo ambatana na
maendeleo.
Post a Comment