Katika kujadili
mada isemayo 'Je ufugaji tunaojihusisha nao unafaa' Mambo mengi yaliibuliwa hapa
na wafugaji hawa na iligundulika kuwa wengi wao:-
-Hawafugi vizuri
ili kupata faida itakayowasaidia kuondokana na umasikini
-Kwa nini
hawafugi vizuri ile hali wanataka faida:- Ukosefu wa malisho ni kikwazo,
ongezeko la mifugo, ukosefu wa elimu ya ufugaji bora, Ukosefu wa mbegu bora nao
ni tatizo.
Wafugaji walipata nafasi kuuliza masali na kujadiliana. |
Mwenyekiti wa Warsha hiyo ambaye vilevile ni mfugaji bw. Paulo msambala mezani akigawa Karatasi zenye maelekezo tosha juu ya Ufugaji bora na Matunzo kwa mifugo pamoja na kanuni na mbinu za kumlinda mnyama dhidi ya maradhi na matibabu yake. |
Afisa Mifugo wa kata ya Kahangara Bi. Dinna Maurice Kasogela akiongoza msafara wa chakula kilichoandaliwa na Kampuni ya Alpha Choice kwaajili ya wafugaji wa kata yake kupata elimu. |
Wafugaji wa vijiji vya kata ya Kahangara wakiwa wamejumuika pamoja kwenye chakula na majadiliano chini kwa chini yakiendelea. |
Post a Comment