Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kitale arithi mikoba ya Sharomillionea



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya na mchekeshaji hapa nchini, Mussa Kitale, amerithi mikoba ya marehemu Hussein Mkiety, Sharomillionea.

Hiyo inatokana na kutesa katika tasnia hiyo, huku macho na masikio ya watu yakielekezwa kwa kijana huyo kila anapokuwapo.

Kitale amekuwa nyota na kupendwa na watu wengi, huku njiani akipita watu kuacha kazi zao na kuanza kumzungumzia yeye, bila kusahau watoto wanaomuunganishia kwa kuanza kumcheka au kumsalimu.

Katika msiba wa Juma Kilowoko, Sajuki, msanii huyo aliongoza kwa kuonwa na watu wengi, wakiwamo watoto ambao muda mwingi walikuwa na shangwe naye.

Kitale alikuwa ndio swahiba mkubwa wa marehemu Sharomillionea, huku msiba huo ukimchoma na kujikuta mara kwa mara akilia, kila akiukumbuka msiba wa msanii huyo aliyefia kijijini kwao Lusanga na kuzikwa huko huko kwa ajali ya gari.

Aina yake kubwa ya uchekeshaji ni kuuvaa uhusika wa uteja na kupeleka ujumbe wake kwa hadhira.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top