Ni kwa namna gani Kristo alijitenga?
E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced. Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple, not as one defeated and forced from the presence of his adversaries, but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the contest”. {DA 620.2}
E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced. Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple, not as one defeated and forced from the presence of his adversaries, but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the contest”. {DA 620.2}
‘Mafarisayo na masadukayo walinyamazishwa. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake, na akawaandaa kuliacha hekalu, sio kama aliyeshindwa na kulazimishwa kuondoka kwa maadui zake, bali kama ambaye kazi yake ilikuwa imekamilika. Alikuwa ni mshindi katika mashindano”. {DA 620.2}
Biblia inasema kwamba Yesu alijitahidi kupingana na mafarisayo na masadukayo akiwa ndani ya mfumo wa dini ya kiyahudi na sasa alikuwa amefikia mwisho wa upinzani wake na akaamua kujitenga moja kwa moja na mfumo wa dini hiyo ili awafundishe vizuri wanafunzi wake ambao walikuwa tayari kukubali mafundisho safi. E.G. White anasema:" Hitherto He had called the temple His Father's house; but now, as the Son of God should pass out from those walls, God's presence would be withdrawn forever from the temple built to His glory. Henceforth its ceremonies would be meaningless, its services a mockery. {DA 620.4}Hatimaye Yesu na wanafunzi wake walijitenga na hekalu lililokuwa mpendwa wao. Lakini kwa sababu viongozi wa hekalu walikataa kufuata mafundisho ya neno la Mungu peke yake, Mwana wa Mungu hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani ya hekalu ingawa “Alikuwa akiliita hekalu kuwa ni nyumba ya Baba yake; lakini sasa, kama Mwana wa Mungu ambavyo akipita kutoka katika kuta hizo, uwepo wa Mungu ungeondolewa milele usionekane ndani ya hekalu lililojengwa kwa utukufu Wake. Hivyo sherehe zilizofanyika ndani ya hekalu hazikuwa na maana, huduma zake zikawa dhihaka”. {DA 620.4}. Hivyo ndivyo alivyofanya Martin Luther na wafuasi wake.
Baada ya kifo cha Martin Luther, wafuasi wake waliendelea katika kufanya matengenezo. Hata hivyo kwa sababu freemasons hawakati tamaa, matengenezo yalikoma na kuanza kurudi nyuma taratibu ambapo leo hii wale wanaoitwa ‘Walutheri’ wameungana tena na mfumo ambao mwanzilishi wao, Martin Luther, aliuiita ‘mfumo mchafu’.
Wakati matengenezo yanaendelea, ulikuwa ni wakati wa kutimizwa kwa unabii wa siku 1260 sawa na miaka 1260 kama ilivyotabiriwa na nabii Yohana. Wakati huo kulianzishwa matengenezo mengi na kupelekea kuanzishwa kwa mifumo mingine ya makanisa. Baadhi ya makanisa yaliyoanzishwa yalikuwa haya:
Anglican: Lilianzishwa huko England na mfalme wa Uingereza ili kupinga kanisa la Roma. Kiongozi mkuu wa kanisa hilo ni Malkia wa Uingereza. Hata hivyo wachunguzi wa dini ya freemasons wanasema kwamba familia ya Malkia ni familia mojawapo kati ya familia 13 za waumini wa Freemasons.
Presbyterian: Mwanzilishi ni John Calvin mwaka 1509 – 1564 na John Knox 1505 – 1572. Kanisa hili lilijitenga na Roma likiwa na motto “Chunguza maandiko” maana liliona kwamba kanisa la Roma linakwenda kinyume na maandiko. Hata hivyo wafuasi wa John Calvin na John Knox wameshindwa kufikia malengo ya kuyachunguza maandiko na kufuata kile asemacho Mungu na badala yake wamekubali kurudi walikotoka!
MENNONITE: Lilizaliwa rasmi mwaka 1525 – 1530 na Conrad Grebel na wenzake akiwemo Zwingli Ulrich aliyetofautiana na Martin Luther juu ya somo la pasaka. Hawa walikataa ubatizo wa Roma wa kunyunyizia maji na jina jingine wanaitwa “Meno Knights” majina ambayo yanafanana na vikundi vya Freemason kama vile “The knights of Eulogia”(Skull and Bones), “The knights of Malta”. Ingawa lengo la Zwingli Ulrich lilikuwa zuri, baada ya kifo chake wafuasi wake walikubali kuingiliwa na freemasons na hivyo kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa.
LUTHERAN: Mwanzilishi ni Martin Luther mwaka 1517. Alikuwa ni Mjerumani aliyesomea ukasisi wa kanisa la Roma na mwaka 1511 akapata Phd katika chuo kikuu cha Wattenberg. Alipingana na kanisa lake la Roma na kuandika sababu 95 zinazopinga mafundisho ya Roma ndipo akajitenga na Roma na hivyo wafuasi wake wakaendelea kutumia jina la Lutheran, yaani wafuasi wa Luther. Wafuasi wa Luther hawakuendelea mbele na sasa wamerudi kwenye makosa aliyokuwa akiyapinga Luther. Je, Lutheran wa leo wanafuata kweli nyayo za Martin Luther? Au wametekwa kwa matumizi ya njama ya “Following Gurus”yaani kufuata kila wasemacho viongozi? Tafakari!
Moravian: Mwanzilishi ni John Huss aliyezaliwa mwaka 1366 na kuchomwa moto na papa hadi kufa mwaka 1416 baada ya kulipinga kanisa la Roma. Wafuasi wake hadi leo wanaitwa kanisa la Moravian. Kwa bahati mbaya wafuasi wa John Huss hawakuendelea kufanya matengezo ili kusonga mbele zaidi ya Huss na kibaya zaidi ni kwamba wanarudi nyuma badala ya kusonga mbele. Leo Huss akifufuka atashangaa kuona jinsi wafuasi wake walivyoacha kanuni alizozianzisha. Je, wamoravian wa leo wako tayari kuchomwa moto kwa kutetea ukweli kama John Huss? Tafakari!
Baptist: Ni kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martin Luther ambao walijitenga na Lutheran mwaka 1600 huko Uholanzi na Uingereza baada ya kuona kwamba wafuasi wenzao wameacha kanuni alizoziweka Martin Luther. Hata hivyo kanisa la Baptist la leo haliendeleza jitihada za Luther na sasa badala ya kusonga mbele linapiga ‘marktime’ likiwa limegeuka nyuma.
Salvation Army (Jeshi la Wokovu): Mwanzilishi ni Booth mwaka 1878. Kanisa hili lilianzishwa na wafuasi wa freemasons kwa lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Kumbuka kwamba Shetani hutumia fursa inayotolewa na Mungu akiwa na lengo la kuwafanya watu washindwe kujua kipi ni cha kweli na kipi sio. Katika kila matengenezo ya kweli, pamekuwepo na matengenezo bandia.
Marmon church: Mwanzilishi ni Joseph Smith (1805 – 1844). Kanisa hili linajulikana pia kama The church of Jesus Christ of later day saints. Kanisa la Mormon lilianzishwa na wafuasi wa freemason wakiwa na lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Mitt Romney ni muumini wa kanisa la Mormon.
Methodist: Kiongozi Mwanzilishi ni John Wesley. Lilianzishwa na watu 17 wa familia moja mwaka 1738 likiwa na lengo la kupinga mafundisho ya freemasons. Kanisa hilo halijakamilisha lengo la matengenezo kutokana na ukweli kwamba wafuasi wake hawana mwamko aliokuwa nao John Wesley.
Watch Tower: Mwanzilishi ni Charles T. Russel 1852 – 1916 na mwenzake J. Lutheford 1869 – 1942. Baba yake Charles T. Russel alikuwa ni mchungaji wa Prebyterian. Mnamo mwaka 1932 huko Marekani jina la kanisa hilo lilibadilishwa na kuitwa Mashahidi wa Yehova. Markus Mpangala ameelezea kwa kirefu chanzo cha dhehebu hili akiainisha kwamba waanzilishi walikuwa ni Freemasons kutoka kwenye familia ya Illuminati inayoitwa Russel illuminati bloodline ambayo nimeshaielezea kwenye makala zilizopita.
Brethen Assemblies: Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na familia ya freemasons.
Makanisa ya Kipentekoste au kilokole: Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya kilokole kama akina T.B Joshua wa SCOAN la huko Nigeria. Kwa wakati huu nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!
Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.
Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.
Seventh –Day Advetist Church: Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya “Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye kanisa hilo likawa chini ya rais wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani. Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na ‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na kazi yake. Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutoka mwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la ‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba kanisa hilo limeingiliwa na freemasons. Wengi wa waumini wa SDA waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’ mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA kwa sababu
Je, madai hayo ni kweli? Tafakari!
Msingi wa kanisa la SDA au ‘Wasabato’ kama inavyojulikana kwa wengi,kuabudu siku ya jumamosi, ni kile kilichoandikwa na Mungu wakati wa uumbaji, kwamba aliumba kwa siku 6 na siku ya 7 akastarehe, akaibariki na akapumzika kisha akawaambia waisraeli: “Ikumbuke siku ya Sabatouitakase….” Kutoka 20:8.
Kutokana na kazi ya chama cha Priory de Sion kwa kuingiza mafundisho machafu ndani ya imani safi, kulitokea utitiri wa makanisa mengi ambayo yanadai kupinga uchafu huo. Hata hivyo wengi wa waumini wa madhehebu hayo ama hawajui asili ya dhehebu lao au hawajui asili ya kile wanachokiabudu. Wengi wamefundishwa na waalimu wa dini na kuwaamini bila hata ya kutaka kuhakikisha kwa akili zao kile wanachofundhishwa. Mungu ametoa nafasi ya kufahamu ukweli kwa kila mmoja wetu bila ya kutegemea viongozi wa dini. Umewahi kufikiri kwamba kama ungekuwa unaishi duniani wewe peke yako, ungemtegemea nani? Tafakari!
Post a Comment