mwenyekiti mteule wa IPC Frank Leonard (kushoto) na katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin kulia tukiteta jambo katika moja kati ya vikao vyetu mwaka jana |
Aliyekuwa mweka hazina wa IPC marehemu Vicky Macha |
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daud Mwangosi na chini siku alipouwawa kinyama |
Klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC) leo imekamilisha kuziba mapengo ya uongozi
yaliyokuwemo ndani ya IPC kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wake
marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa tarehe 2/9/2012 Nyololo katika vurugu za
polisi na Chadema, pia nafasi ya mweka hazima wake mkuu Vicky Macha
aliyefariki mwezi wa 10/2012 pamoja na nafasi za wajumbe watatu wakamati
ya utendaji .
katika uchaguzi huo
uliofanyika leo wakati wa mkutano maalum wa uchaguzi wa IPC uliofanyika Hotel
ya M.R mjini Iringa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Frederick Siwale
aliwataja waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji wa IPC
Frank Leonard aliyepata kura 17 kati ya kura 18 zilizopigwa katika nafasi
hiyo ya uenyekiti iliyokuwa ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari
aliyetangaza kujitoa na kuomba wajumbe kumchagua Leonard kutokana na utendaji
wake mzuri , wakati makamu mwenyekiti amepita bila kupingwa Jackson Manga
aliyepata kura zote 18 za wajumbe wa mkutano huo ambao jumla ya wanachama
hai wa IPC ni 24 ila waliofika leo ni 18 wakati nafasi ya katibu mtendaji
wa IPC imechukuliwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa IPC Francis Godwin
aliyepata kura za ndio 16 huku kura 2 zikimkataa .
Wengine waliochaguliwa
ni pamoja na mweka hazina mkuu wa IPC Janeth Matondo aliyechukua nafasi ya
marehemu Vicky Macha kwa kupata kura zote za ndio 18 pamoja na mweka hazina
msaidizi Suleiman Boki aliyepata kura zote 18 .
Wajumbe watatu
waliochaguliwa ni Hapy Matanji aliyepata kura (18) Swiga Mwaisumbe (18 ) na
Selina Ilunga(17).
Na Francis
Godwin
Post a Comment