Kikosi cha Wachezaji 28
na viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kuwasili mchana wa leo kwa ndege ya shirika la Afrika
Kusini, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius kambarage
Nyerere.
Kikosi cha Wachezaji 28 na
viongozi 11 wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya waratibu wa shindano hilo,kutoka kampuni ya Prime Time
Promotions Ltd,Pichani kushoto ni Shaffih Dauda,Mmoja wa Wakurugenzi wa Prime
Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga,Mtangazaji wa kipindi cha Sports Extra,Mbwiga
Mbwiguke,Mdau Juma pamoja na Stuart
Nahodha wa timu ya Black
Leopards ya Afrika Kusini akizungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali
mara baada ya kuwasili na kikosi chake kizima leo mchana tayari kwa kupambana na
timu ya Yanga Sports Club,kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar.
Waratibu kutoka Prime Time
Promotions Ltd,Shaffih Dauda pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo
Godfrey Kusaga wakifanya mawasiliano leo mchana mara timu ya Black Leopards ya
Afrika Kusini ilipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
J.K.Nyerere..
Shaffih Dauda akiwa
ameambatana kocha wa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,Abel Makhubele
mara baada ya kuwasili leo mchana kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu J.K.Nyerere.
Wachezaji wa timu ya Black
Leopards ya Afrika Kusini,wakiingia kwenye basi kubwa la timu ya
Yanga,wayatarajia kumenyana nayo hapo kesho kwenye uwanja wa Taifa,Jijini
dar.
Kikosi cha Wachezaji 28 na viongozi 11 wa timu ya
Black Leopards ya Afrika Kusini,wakiwasili mapema leo mchana kwa ndege ya
shirika la Afrika Kusini, kwenye uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. kambarage Nyerere.Picha zote na JIACHIE
BLOG.
WAKATI mabingwa wa soka wa
Afrika Mashariki na Kati, Yanga kesho watacheza mechi ya kwanza ya
kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, kocha wa
Black Leopards ametema cheche na kusema wataibuka na ushindi mkubwa kutokana na
uzoefu wao wa mashindano ya Kimataifa.
Mchezo huo umepangwa kuanza
saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha kamilika huku waandaaji
wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki wengi
kufika.
Mratibu wa mechi hiyo,
Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa maandalizi yote
yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha shs 5,000 na shs 7,000 na kuwa cha shs
3,500 ili kuwafanya mashabiki wengi kuona mechi hiyo.
Viingilio vingine ni shs
7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni shs 15,000 , VIP B shs
20,000 na VIP A shs 30,000
Dauda alisema kuwa Black
Leopards wamewasili na kutamba kushinda mechi hiyo kutokana na uzoefu waliopata
katika mashindano mbali mbali ikiwa pamoja na kombe la
Shirikisho.
Kocha wa timu hiyo, Abel
Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na walifanya ziara nchi mbali
mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja ya faraja
kwao.
“Ziara hii ziara yetu ya
kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na nchi nyingie, tulipata
matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata matokeo mazuri hapa, nimekuja na
wachezaji wangu wote wa kikosa cha kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki
watarajie mchezo mzuri,” alisema Makhubela.
Alisema kuwa wanaijua
Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la Afrika na hivyo
wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao ambayo ipo
katikati..
Post a Comment