Kibanda cha Hoteli ya Palumbo
Reef iliyopo Uroa kinachotarajiwa
kuunganishwa na Jeti inayoelekea Baharini kwa ajili ya michezo ya Watalii wa Hoteli
hiyo.
Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,
akiangalia ramani ya mchoro wa jeti inayotaka kujengwa na Hoteli ya Palumbo Reef
kutoka kwa mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana Palumbo Sila (kulia) wakati
alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea maandalizi hayo, leo asubuhi, mjini
Zanzibar.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Hoteli
ya Palumbo Reef mara baada ya kutembelea eneo linalotaka kujengwa jeti kwa ajili
ya wakatii wa Hoteli hiyo. Kati
kati yao aliyevaa nguo nyeupe ni mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana Palumbo
Sila.-
*****
Makampuni
na Taasisi zinazojihusisha na masuala ya uwekezaji katika Sekta ya Utalii
yametakiwa kuzingatia taratibu za tathmini ya kimazingira kabla ya
kuanzishakwa miradi
yao kwa lengo la kujilinda na uchafuzi wa Mazingira pamoja na rasilmali za
Taifa.
Nasaha
hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara
baada ya kutembelea eneo lilalotaka kujengwa Jeti itakayopitisha watalii kwa
ajili ya michezo ya Baharini ambalo
limelalamikiwa na Idara ya Mazingira Zanzibar kukiuka Taratibu
za kimazingira katika
Hoteli ya Palumbo Reef iliyopo Uroa Wilaya ya
Kati.
Balozi
Seif alisema Hoteli au mradi wowote wa kitalii unaotaka kuwekezwa Nchini lazima
uzingatie na kukubalika kufanyiwa tathmini ya kimazingira na Taasisi inayohusika
na masuala hayo ambayo ni idara ya
mazingira.
Alisema
upo wasi wasi unaoonekana wazi wa bahari kuendelea kula eneo kubwa la ardhi
kutokana na uchafuzi wa mazingira ambao kwa kiasi kikubwa unasababishwa na tabia
ya baadhi ya watu wasiozingatia utunzaji wa
mazingira.
“ Huu ni
utaratibu uliowekwa kisheria na Serikali. Hivyo lazima kwa uongozi wowote wa
taasisi ya uwekezaji katika sekta ya Utalii ufuate taratibu ya Idaya ya
Mazingira pamoja na Taasisi ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } ili
kuwepuka mapema matatizo kama hayo”. Alifafanua Balozi
Seif.
Akizungumzia tatizo la
ardhi linalolalamikiwa na Wananchi wa Uroa dhidi ya Uongozi wa Hoteli hiyo ya
Malumbo Reef Balozi
Seif alisema Zanzibar hivi sasa imechoshwa na haihitaji tena kuendelea kuwa na
migogoro ya ardhi.
Alisema
Serikali imefikia uamuzi wa sehemu ya ardhi yake ndogo iliyonayo kutumiwa kwa
ajili ya sekta ya Utalii ili kusaidia Uchumi wa Taifa ambao bado unategemea zao
la Karafuu na migogoro iliyopo sasa lazima ifuatiliwe na kutafutiwa suluhisho la
kudumu.
Balozi
Seif alisisitiza kwamba mategemeo ya Taifa kwa ujumla ni kuona mapato yatokanayo
na sekta ya Utalii yanaifaidisha Serikali sambamba na wananchi wote badala ya
kuona neema hiyo inakwenda na kuingia mikononi kwa muekezaji
pekee.
“Mapato ya
Utalii lazima yaifaidishe Serikali ambayo ndio iliyoamua kutumia ardhi yake
chache iliyokuwa
nayo kwa kupanua sekta ya utalii kwa mategemeo ya kuongeza mapato
kwa wadau wote wa sekta hiyo”. Alisisitiza Balozi
Seif.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Hoteli ya Palumbo Reef kwa
juhudi zake za kuwa karibu na wananachi wa eneo hilo hali inayojenga mazingira
mazuri ya uwekezaji katika sekta ya Utalii kati ya wageni na wenyeji
husika.
Mapema
Mkurugenzi wa Hoteli ya Palumbo Reef Bwana Shaaban Haji
Kitwana alisema tatizo kubwa linalojitokeza ambalo hata halihitaji ufumbuzi wa
ngazi za juu za Serikali ni
kwa baadhi ya wazawa kuwa na tabia chafu ya kuwahadaa
kimaarifa wenzao wakati wanapouza mali zao kwa ajili ya
uwekezaji.
Bwana
Shaaban alisema ipo
mikataba wanayokubaliana na Wananachi hao inayofikia maamuzi sahihi lakini
baadaye huchipuka mzozo kati ya wazawa hao na hjatimae kuwahusisha wawekezaji
wasiostahiki kuwemo kwenye mzozo huo.
Naye kwa
upande wake Mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana Palumbo Sila alimueleza
Balozi Seif kwamba mazingira na ukarimu uliopo Zanzibar ndio chachu
inayowahamasisha wawekezaji wengi wa nje kuja kuwekeza vitega uchumi vyao hapa
Nchini.
Bwana
Mapumbo alisema katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na tatizo
la ajira
Uongozi wa Hoteli hiyo umeamuwa
kuwapa kipaumbele Wananchi
Wazalendo katika
shughuli za uendeshaji wa Hoteli hiyo kwa zaidi ya asilimia
99.9%.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/1/2013.
Post a Comment