KWA kutumia mabango, lengo likiwa kutangaza kazi zao,
waganga wengi wa tiba asilia wamekuwa wakijinadi kuwa wanatoa tiba ya kurefusha
maumbile ya siri ya wanaume, kukuza makalio au
matiti.
Katika mitaa ya miji na majiji nchini, siyo jambo la
ajabu kukutana na mabango hayo, ambayo hata hivyo kushamiri kwake kunaleta picha
kwamba ni kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo nchini, huku watoa huduma
husika wakinufaika kwa kujikusanyia kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa
wahitaji.
Pia dawa zinazodaiwa kukuza makalio maarufu kama
‘mchina’, zimekuwa gumzo baada ya kuingia nchini, huku zikielezwa kukosa ubora
na kwamba zina madhara makubwa.
Lakini, sasa unaweza kuachana na dawa hizo za Kichina,
baada ya kugundulika mmea wenye uwezo wa kukuza makalio, matiti, pamoja na
kurefusha uume.
Taarifa za kiutafiti zinautaja mti huo kwa jina la
Mvunge, ukiwa na uwezo wa kukuza makalio, matiti na kurefusha
uume.
Kaimu Msajili wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, Dk
Naomi Mpemba anasema kuwa mmea huo ambao huwa ni mti mkubwa upo na kwamba una
uwezo mkubwa wa kukuza maumbile hayo.
Anabainisha kuwa mmea huo ambao hukua na kuwa mti
mkubwa huzaa matunda yanayotumika kama dawa na unapatikana wilayani Korogwe Mkoa
wa Tanga, Pwani, Mbeya, Morogoro na baadhi ya mikoa
nchini.
“Tulifuatilia na kutambua kuwa mti huo upo maeneo hayo
na unatumiwa zaidi na waganga, hata picha za mti huo tunazo,” anasema Dk Mpemba
na kuongeza:
“Jina jingine unaitwa Miegeya, mara nyingi unastawi
katika maeneo yenye ardhi ya unyevunyevu, una tabia ya kustawi kama Mwembe na
matunda yake huonekana kufanana na Mbuyu
Post a Comment