Wanachama wa CCM tawi la chuo cha Mkwawa wakiwa na mabango mkatika mapokezi ya mangula leo |
Umati wa wana CCM waliofika uwanja wa Mwembetogwa kumsikiliza Mangula |
Makamu mwenyekiti wa CCM bara Philip mangula katikati akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza kulia |
Huku wanafunzi wa
chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa wakimpokea Mangula kwa mabango yenye
jumbe mbali mbali ukiwemo wa kumpongeza Mangula kwa kuteuliwa na ule
unaolalamikia utaratibu mbovu wa ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi hao
wa vyuo vikuu pamoja na kuitaka CCM kukomesha vitendo vya rushwa ndani na
nje ya chama.
Katika historia ya CCM
jimbo la Iringa na mkoa wa Iringa haijapata kutokea mapokezi ya kishindo kama
hayo baada ya umati mkubwa wa wananchi kujitokeza kumpokea Mangula huku
maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa yakipambwa kwa bendera za CCM mithiri
ya makao makuu ya CCM Dodoma wakati wakati wa mkutano mkuu wa chama
hicho.
Wakizungumzia juu ya
mapokezi hayo ya kishindo kwa Mangula baadhi ya wananchi wameonyesha
kutofautiana juu ya mapokezi hayo huku baadhi yao wakidai kuwa maandalizi ya
mapokezi hayo yamefanywa na Jesca Msambatavangu ambae ni mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Iringa ambae ni mwanamke wa kwanza kuongoza chama hicho toka nchi
ilipopata uhuru wake mwaka 1961 huku wengine wakidai kuwa ni matokeo ya
kukubalika kwa sekritaeliti mpya ya CCM akiwemo katibu mkuu wa CCM na
mwenyekiti na makamu wake bara na visiwani.
Katibu wa umoja wa
vijana wa CCM mkoa wa Iringa Rhoda George alisema kuwa wananchi wa jimbo la
Iringa mjini wamejitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo kutokana na
utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM unaofanywa na madiwani wake pamoja na
wabunge wa CCM mkoa wa Iringa.
Hata hivyo alisema
kuwa mapokezi hayo makubwa kwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini ni ishara
nzuri ya ushindi wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na
uchaguzi mkuu mwaka 2015 katika jimbo hilo.
Kwa upande wake Brown
Payovela alisema kuwa wakazi wa mkoa wa Iringa wameonyesha matumaini
makubwa kwa Mangula na kuwa upo uwezekano mkubwa wa CCM kuendelea kushinda
kwa kishindo katika chaguzi zake zijazo.
Baadhi ya wananchi
mashabiki wa vyama vya upinzani mjini Iringa walisema kuwa CCM imetumia mbinu
ya kunyong'onyeza nguvu ya vyama vya upinzani katika jimbo hilo la Iringa
mjini hasa chama cha Chadema ambacho mbunge wake ni mchungaji Peter Msigwa
.
Hivyo walisema kuwa
iwapo mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa hatafanya kazi zinazoonekana
uwezekano wa kuambulia kura mwaka 2015 unaweza kuwa mdogo japo walisema
kuwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 upinzani bado utategemea huruma za wana
CCM kuendelea kumchagua mbunge huyo ila iwapo CCM itafanya mchezo mchafu
katika utaratibu wa kumpata mgombea wa ubunge jimbo hilo.
Alisema Damas Kalinga
mkazi wa Kihesa ambaye alijitambulisha kuwa ni shabiki wa Chadema kuwa hadi
sasa ndani ya CCM jimbo la Iringa mjini tayari wagombea wameanza
kuwachanganya wananchi kwa kila mmoja kuonyesha kuitaka nafasi ya ubunge na
kuwataka viongozi wa CCM kuwa makini zaidi.
Miongoni mwa wabunge
waliojitokeza katika mapokezi hayo ni pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa
wa Iringa Ritta kabati , mbunge wa jimbo la kalenga na waziri wa fedha Dr
Wiliam Mgimwa,makada wa CCM pamoja na wakuu wa wilaya za Iringa , Kilolo na
Mufindi wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine
Ishengoma.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jasca Msambatavangu akimkaribisha Mangula
katika uwanja huo wa Mwembetogwa kwa ajili ya kuwahotubia mamia ya
wananchi waliofika katika uwanja huo alisema kuwa CCM itaendelea kueleza
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa wananchi wake na kuwa tayari baadhi ya
kata zimeanza kutoa utekelezaji wa ilani hiyo kwa
wananchi.
Msambatavangu
aliwapongeza wanachama wa vyama vya upinzani ambao wameanza kurudi CCM na
kuwa kurejea kwa wanachama hao wa vyama vya upinzani ndani ya CCM ni kutokana
na utekelezaji mzuri wa ilani yake kwa wananchi na uendeshaji wa CCM ndani ya
CCM bila kunadi sera za matusi na ubaguzi
.
Post a Comment