
Unakumbuka nani alikuwa wa
pili wakati Iniesta anakuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012? Iniesta
hakufuatwa na mtu mmoja nyuma yake, walikuwa wawili nao ni Messi na Cristiano
Ronaldo, hawa walikuwa wa pili kwenye tuzo hiyo kwa sababu kura walizopigiwa
zililingana. Wakati tukiwa tunangojea kutangazwa kwa mchezaji bora wa dunia
baada ya masaa machache, mambo yamebadilika Iniesta bado yupo kwenye
kinyang’anyiro hicho lakini si mtu anayepewa nafasi kubwa ya kuwa namba moja
tena, nafasi yake ni ya tatu kulingana na na maoni ya wadau wengi, kitu ambacho
binafsi naafiki moja kwa moja lakini pia naamini lolote laweza kutokea. Sasa
bado utata upo kwenye nani ataishika namba moja?
Basi tuwaangalie
Messi, Iniesta na Ronaldo kwa ukaribu katika mwaka
2012;
Messi
Nakuhakikishia asilimia zaidi ya 60 ya watanzania
wapenda soka wakiulizwa wao watamchagua nani ashinde tuzo ya mchezaji bora wa
dunia kwa sasa, watamchagua huyu, unajua kwa nini? Messi ndiye mwanasoka
anayetajwa zaidi kwenye vyombo vya habari kwa hivi sasa hii inatokana na rekodi
ambazo amekuwa akizivunja kila kukicha. Rekodi nyingi za ufungaji katika soka
sasa zinashikiliwa naye. Tayari Messi ameshashinda tuzo hii mara tatu mfululizo
je atafanya hivyo tena kesho? Lolote linawezekana, lakini si watanzania pekee
wanaomuona Messi kama ndiye mchezaji bora bali hata vyombo vingi vya habari
duniani pia vimekuwa vikimpigia chapuo la kuibuka
kidedea.
Iniesta
Kama nilivyosema hapo mwanzo, Iniesta ndiye mchezaji
bora wa Ulaya kwa hivi sasa, na ndiye mchezaji bora waligi ya mabingwa Ulaya kwa
msimu uliopita na michuano ya kombe la Ulaya kwa mwaka 2012. Iniesta ni mchezaji
mwenye kipaji cha hali ya juu yeye huuchezea mpira vile anavyotaka yeye. Si
mfungaji sana lakini ni mtoa pasi za magoli mzuri sana. Iniesta ni moja ya mazao
adhimu sana kutoka La Masia, wengine ni Messi na Xavi Hernandes. Je mchezaji
bora wa Ulaya atakuwa mchezaji bora wa dunia hapo kesho? Tungoje kidogo tu,
kesho si mbali.
Ronaldo
Jose Mourinho, kocha wa Real Madrid aliwahi
kusema kuwa kama Messi ni mchezaji bora wa dunia basi Ronaldo ndiye mchezaji
bora wa ulimwengu. Kwa mwaka 2012, mambo mengi ya Cristiano yalienda vizuri,
yeye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Hispania, La Liga baada ya kuiwezesha
Real Madrid kushinda ligi kuu kwa jumla ya pointi 100, pia Ronaldo aliiwezesha
Ureno kufika nusu fainali ya kombe la Ulaya huku yeye akiwa ndio mwezeshaji mkuu
kufikia mafanikio hayo. Mancini, kocha wa Manchester City alisema wanahitaji
polisi kumdhibiti Ronaldo wakati City ilipokuwa ikienda kupambana na Madrid
kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. Ronaldo pia anapewa nafasi na wachezaji na
makocha wengi maarufu. Je Ronaldo atawapiku Messi na Iniesta? Masaa machache tu
yamebaki wadau

Unakumbuka nani alikuwa wa pili wakati Iniesta anakuwa mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2012? Iniesta hakufuatwa na mtu mmoja nyuma yake, walikuwa wawili nao ni Messi na Cristiano Ronaldo, hawa walikuwa wa pili kwenye tuzo hiyo kwa sababu kura walizopigiwa zililingana. Wakati tukiwa tunangojea kutangazwa kwa mchezaji bora wa dunia baada ya masaa machache, mambo yamebadilika Iniesta bado yupo kwenye kinyang’anyiro hicho lakini si mtu anayepewa nafasi kubwa ya kuwa namba moja tena, nafasi yake ni ya tatu kulingana na na maoni ya wadau wengi, kitu ambacho binafsi naafiki moja kwa moja lakini pia naamini lolote laweza kutokea. Sasa bado utata upo kwenye nani ataishika namba moja?
Basi tuwaangalie Messi, Iniesta na Ronaldo kwa ukaribu katika mwaka 2012;
Messi
Nakuhakikishia asilimia zaidi ya 60 ya watanzania wapenda soka wakiulizwa wao watamchagua nani ashinde tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa sasa, watamchagua huyu, unajua kwa nini? Messi ndiye mwanasoka anayetajwa zaidi kwenye vyombo vya habari kwa hivi sasa hii inatokana na rekodi ambazo amekuwa akizivunja kila kukicha. Rekodi nyingi za ufungaji katika soka sasa zinashikiliwa naye. Tayari Messi ameshashinda tuzo hii mara tatu mfululizo je atafanya hivyo tena kesho? Lolote linawezekana, lakini si watanzania pekee wanaomuona Messi kama ndiye mchezaji bora bali hata vyombo vingi vya habari duniani pia vimekuwa vikimpigia chapuo la kuibuka kidedea.
Iniesta
Kama nilivyosema hapo mwanzo, Iniesta ndiye mchezaji bora wa Ulaya kwa hivi sasa, na ndiye mchezaji bora waligi ya mabingwa Ulaya kwa msimu uliopita na michuano ya kombe la Ulaya kwa mwaka 2012. Iniesta ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu yeye huuchezea mpira vile anavyotaka yeye. Si mfungaji sana lakini ni mtoa pasi za magoli mzuri sana. Iniesta ni moja ya mazao adhimu sana kutoka La Masia, wengine ni Messi na Xavi Hernandes. Je mchezaji bora wa Ulaya atakuwa mchezaji bora wa dunia hapo kesho? Tungoje kidogo tu, kesho si mbali.
Ronaldo
Jose Mourinho, kocha wa Real Madrid aliwahi kusema kuwa kama Messi ni mchezaji bora wa dunia basi Ronaldo ndiye mchezaji bora wa ulimwengu. Kwa mwaka 2012, mambo mengi ya Cristiano yalienda vizuri, yeye alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Hispania, La Liga baada ya kuiwezesha Real Madrid kushinda ligi kuu kwa jumla ya pointi 100, pia Ronaldo aliiwezesha Ureno kufika nusu fainali ya kombe la Ulaya huku yeye akiwa ndio mwezeshaji mkuu kufikia mafanikio hayo. Mancini, kocha wa Manchester City alisema wanahitaji polisi kumdhibiti Ronaldo wakati City ilipokuwa ikienda kupambana na Madrid kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. Ronaldo pia anapewa nafasi na wachezaji na makocha wengi maarufu. Je Ronaldo atawapiku Messi na Iniesta? Masaa machache tu yamebaki wadau


Post a Comment