Kwa mara ya kwanza juzi january 10 2013 ndio zilitangazwa habari za msanii Mh Temba kuibiwa vitu vya gari lake kwa mara ya tano, amekua na magari tofauti tofauti ambapo kwa mara tano ameibiwa vitu mbalimbali ambapo baadae amekua akilazimika kununua vitu vilevile vya kwake.
Huyu jamaa anatuhumiwa kuwa mwizi hodari wa power window, vioo na vifaa vingine vya magari mbalimbali ambapo alipohojiwa na polisi amesema yeye huwa ananunua tu vifaa vya magari lakini hausiki kufanya wizi.
Wanaofanya wizi ni wengine ndio wanamletea na yeye anafanya kazi ya kumpigia simu mwenye mali ili aje avinunue vifaa vilivyoibiwa kwenye gari lake, sasa kilichofanya Mh Temba amkamate ni pale alipopigiwa simu na huyu huyu jamaa na kudai kwamba anavyo vifaa vilivyoibwa kwenye gari lake.
Kumbe huyu jamaa ndio yule yule aliwahi kumpigia simu Temba wakati alipoibiwa tena vifaa vya gari november 2012 na kumuuzia vifaa vilevile kwa shilingi laki nane huku Temba akiitoa hiyo pesa akiwa anajua kabisa vifaa anavyonunua ni vilevile, wakati huu Temba bado alikua ameisave namba yake kwa hiyo akashtukia mchezo kwamba jamaa ndio wanamchezea hivyo akajipanga na kwenda kumkamata.
Mtuhumiwa alipofikishwa polisi akajitetea kwamba yeye hausiki na wizi, yeye anafanya udalali wa kununua na kuuza hivyo vifaa tu na wala vitu vingine vinavyoibwa kwenye magari kama Camera na Laptop huwa hausiki navyo na wala havinunui.
Polisi wanamjua kabisa na namba yake wanayo kwa sababu jamaa amekua na kesi hizo mara nyingi sana hapo kituoni, mara ya mwisho ambapo wengi wanaoibiwa vifaa huwa anawaambia watume pesa kupitia line yake ya simu ya mkononi alafu wakishatuma ndio mtu anatumwa kwenda kuvipeleka hivyo vifaa, kama alivyofanya kwa Mh Temba mara ya mwisho na alitaka kufanya hivyo hata wakati huu.
Mh Temba amerudishiwa vifaa vyake alivyoibiwa wakati huu na mtuhumiwa ameachiwa, sio kwa dhamana ila wamechukua tu alama zake za vidole wakamwambia arudi jumatatu, Temba nae kaambiwa arudi jumatatu.

Post a Comment