Jeshi la Polisi Mkoani
Geita limefanikiwa kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni kumi na Tisa zilizokuwa
katika Taasisi ya Kifedha ya FINCA Mkoani humo, baada ya taasisi hiyo kuvamiwa
na Majambazi watano wakiwa na silaha za moto na mabomu ya kienyeji kwa lengo la
kufanya uporaji.
Akieleza tukio hilo Kamanda
wa Polisi Mkoani Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi Leonard Paulo alisema tukio
la kuvamiwa kwa Taasisi hiyo kulitokea Januari kumi na mbili majira ya saa saba
usiku ambapo Majambazi hao walivunja mlango wa Nyuma wa Ofisi hizo kwa kutumia
bomu la kienjeji na kumjeruhi kwa risasi mlinzi wa ofisi hiyo Rajabu Muhoja
(28).
Alisema baada bomu hilo
kutumika Askari waliokuwa doria walisikia mlipuko na ndipo walipofika eneo hilo
na kuanza mapambano ya kurushiana Risasi na majambazi ambapo baada ya majambazi
kuzidiwa nguvu yalikimbia na kuacha kiasi hicho cha fedha zilizokuwa katika
ofisi hiyo.
Kamanda Paulo alisema
Majambazi hayo yalifanikiwa kuondoka na kompyuta mpakato (Laptop) mbili na
juhudi za kuwasaka zinaendela ambapo Zawadi nono itatolewa kwa mtu yeyote
atakayesaidia kutoa taarifa za kukamatwa kwa majambazi
hayo.
Aidha alisema katika eneo
la tukio kumekutwa bomu la kienyeji na viroba viwili vya mchanga unaotumika
kutengeneza mabomu ya kienyeji na hali ya Mlinzi aliyejuruhiwa inaendelea
vizuri.
Post a Comment