Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

POLISI ARUSHA WAKUSANYA BILIONI 1.2 KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI

Liberatus-Sabas

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limefanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 1.2 kwa mwaka 2012 ambapo mwaka jana jeshi hilo lilikusanya zaidi ya Milioni 518 kutokana na makosa mbalimbali ambayo yanatozwa mara baada ya wananchi kuvunja sheria za Jeshi hilo
Akiongea na “FULL SHANGWE”jana kuhusuniana na mapato ya jeshi hilo kwa mkoa wa Arusha kamanda wa polisi mkoani hapa Liberatus Sabas alisema kuwa kuongezeka kwa fedha hizo kunatokana na jitihada mbalimbali za jeshi hilo za kupambana na uhalifu.

Sabas alisema kuwa mbali na jeshi hilo kuweza kupambana na uhalifu hivyo kukusanya kiwango kikubwa sana cha fedha lakini hata uhalifu wenyewe, ajali za barabarani nazo zimepungua tofauti na miaka ya nyuma kutokana na jitiada ambazo zinafanywa na Polisi
Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2011 matukio ya ajali za barabarani yalikuwa ni 2507 wakati mwaka 2012 matukio yatokanayo na ajali yalikuwa ni 2106 sawa na upungugu wa asilimia 16
Akiendelea kuelezea pia alisema kuwa hata matukio ya vifo vitokanavyo na ajali navyo vimepungua kwa kiwango cha hali ya juu sana ambapo kwa mwaka 2011 matukio yalikuwa 211 huku 2012 yalikuwa ni 175 sawa na upungufu wa asilimia 17 ambapo hali hiyo imetokana na Jitiada mbalimbali ambazo zinatokana na Jeshi hilo
Mbali na hayo pia makosa ya barabarani ambayo yamelipiwa nayo yamechangia sana kuinua pato letu la mwaka ambapo yalikuwa ni zaidi ya elfu 42 kwa mwaka 2012 tofauti na mwaka 2011 ambapo makosa hayo yalikuwa ni 1978 sawa na ongezeko la makosa ya barababarani yaliyolipiwa kwa asilimia 119
Kutokana na hali hiyo Kamanda Sabas aliwataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanakuwa walindaji wazuri wa sheria za nchi na wala sio wavunjaji wazuri wa sheria za Nchi kwani uvunjwaji wa sheria za nchi ndio chanzo cha vifo ,Umaskini pamoja na Migogoro mikubwa sana ndani ya jamii.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top