Rais Yoweri Museveni wa
Uganda ameweka wazi kuwa serikali yake inakusudia kujenga kujenga nyumba kwa
ajili ya waalimu na madaktari katika maeneo yao ya kazi.
Akizungumza alipotembelea
shule ya Sekondari ya Kazo iliypo wilaya ya Kiruhura rais huyo aliyekuwa
ameambatana na mkewe, ameahidi kutoa msaada wa basi katika shule hiyo ya
mchanganyiko.
Chini ya Mpango wa Elimu ya
Sekondari kwa Wote, serikali imetumia jumla ya shilingi milioni 565 kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa 12 na maabara 2 za kisayansi katika shule
hiyo.
Aidha asema kuwa serikali
itajenga darasa la kompyuta na maktaba shuleni
hapo.


Post a Comment