Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Bw. Absolom Kibanda akimkabidhi maoni ya Jukwaa hilo kuhusu
katiba Mpya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika
ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Jan 10, 2013)
.
Mwanachama wa Jukwaa la
Wahariri (TEF) Bw. Deodatus Balile akiwasilisha maoni ya Jukwaa hilo kuhusu
Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam
leo (Alhamisi, Jan 10, 2013). Wengine ni Bw. Ruge Mutahaba (kushoto) kutoka
Clouds Media Group na Bw. Yasin Sadik kutoka gazeti la Hoja.
Katibu Mtendaji wa
Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akiwasilisha maoni ya
Baraza hilo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume
jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Jan 10, 2013). Kulia ni Bi. Pili Mtambalike
kutoka MCT.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT) Bw. Reginald Mengi akitoa maoni ya chama
hicho kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo
(Alhamisi, Jan 10, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mjumbe wa Tume hiyo Prof. Palamagamba Kabudi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Valerie Msoka
akikabidhi maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume hiyo jijini Dar
es Salaam leo (Alhamisi, jan 10, 2013).Wnaoshuhudia ni Wajumbe wa Tume, Dkt.
Salim Ahmed Salim, Bw. Simai Mohammed na Bi. Jessica
Mkuchu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Valerie Msoka akitoa
maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi
za Tume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Jan 10, 2013).
Mmoja wa Wawakilishi wa Kundi la Wafugaji waliokutana na Tume
ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan. 10, 2013) Bi. Lilian
Looloitai akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume, jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Bw. Adam Ole Mwarabu na kushoto ni Bw. Joseph
Parsambei.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakifuatilia mkutano kati yao na
Wawakilishi wa Wafugaji uliolenga kupata maoni ya kundi hilo kuhusu
Katiba Mpya. Kutoka kushoto ni Bi. Maria Kashonda, Dkt. Senondo Mvungi
na Bw. Yahya Msulwa.
Mmoja wa Wawakilishi wa Kundi la Wafugaji waliokutana na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Alhamisi, Jan. 10, 2013) Bi. Esta
Labani akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume, jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya Wawakilishi wa Wafugaji waliokutana na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba leo (Alhamisi, Jan. 10, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya wakifuatilia mkutano.
Post a Comment