WATANZANIA wametakiwa kuutumia mwaka 2013 kuwa wakujieleimisha na kuchukua hatua ya kupima afya zao, kubaini mapema kama wamekumbwa na saratani ya tezi dume, matiti na shingo ya uzazi, hali itakayosaidia kutibu maradhi hayo kwa haraka.
Kauli hiyo ilitolewa
jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa ‘Tanzania 50 Plus Campaign, Mchungaji Dk
Emmanuel Kandus, wakati alipokuwa akitoa ujumbe wa mwaka mpya kuhusu hali halisi
ya maradhi hayo, jinsi yanavyoshika kasi kila kukicha.
“Tunashudia watu wengi
wamekuwa wakitumiana vimeseji vya kutakiana heri na Baraka za mwaka mpya
wakiasana hili na lile ili mradi kuukaribisha mwaka mpya”alisema Dk.
Kandus.
Alisema Taasisi hiyo
imeamua kutoa ujumbe huo, kwa kuwakumbusha kuwa gonjwa saratani kwa sasa ni
gonjwa tishio kwa maisha ya watu wengi duniani, katika nchi zinazoendelea
hususani Afrika katika nchi zilizoko chini ya jangwa la Sahara, Tanzania ikiwa
miongoni mwa hizo huku ikiwa na hali mbaya sana.
Dk. Kandusi alisema takwimu
duniani zinaonyesha kuwa mwaka 2010 malaria iliua watu 500,000, kifua kikuu
milioni 2.1, ukimwi million 1.8 na saratani million 9.9.
Alibainisha kuwa asilimia
75 ya vifo vya watu hao milioni 9.9, ambapo milioni 7.4 walifariki toka nchi
zinzoendelea.
Dk Kandusi alisema
inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2020 malaria itaua watu milioni 2.5, kifua kikuu
milioni 2.2, ukimwi milioni 1.5 na saratani milioni 12.2.
Dk Kandusi alitoa wito kwa
wananchi kuwa wakati tunapoingia mwaka 2013 kuliangalia gonjwa la saratani kwa
ukaribu na umakini.
Naye Prof. Twalibu ngoma,
Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Ocean Road Cancer Institute’, katika mahojiano yake hivi
karibuni na kituo kimoja cha Televisheni, alinukuliwa akisema kuwa watu 100
wanakufa kila siku nchini kutokana na ugonjwa huo wa
saratani.
Itakumbukwa aliyekuwa
Waziri wa Afya, Prof. David Homeli Mwakyusa alinukuliwa akisema watu wengi
huugua ugonjwa huo lakini ni asilimia 10 ya wagonjwa saratani ndio wanaofika
hospitali kwa tiba ya saratani ambapo asilimia 90 huugua na kupoteza maisha yao
bila kufika hospitalini.
Post a Comment