Picha juu na chini ni Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt
Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za
Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa
hoteli hiyo kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza
mazingira.
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro imeamua kuialika
kampuni ya usafi ya Green Waste Pro baada ya kuona juhudi zao za kuweka Manispaa
ya Ilala safi na mabadiliko yanaonekana ndipo wakaamua kushirikiana nao katika
zoezi la kusafisha fukwe hizo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana
na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini
Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo
iliyojipangia kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza
mazingira.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro
ltd Bw. Abdallah Mbena (kushoto) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika fukwe
za Kivukoni Front baada ya kupata mwaliko kutoka Hoteli ya Hyatt Regency wa
kushiriki katika kusafisha fukwe hizo.
Mwananchi asiyefahamika akiwa amechapa usingizi huku
akiwa amejifunika gunia chafu na kulifanya kuwa shuka katika kichaka cha fukwe
za Kivukoni Front wakati zoezi la usafi likiendelea.WADAU huyu jamaa hatuna
uhakika kama naye ni sehemu ya uchafu au ndio nyumbani?? Tembea
uone.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Hoteli
ya Hyatt Regency Kilimanjaro wakiwa wamebeba mafurushi ya lundo la uchafu
uliokusanywa kutoka kwenye fukwe za Kivukoni Front zilizopo karibu na Hoteli
hiyo.
Moja ya magari ya kukusanya uchafu ya kampuni ya Green
Waste Pro likiwa limesheheni lundo la uchafu uliokusanywa toka kwenye Fukwe za
Kivukoni Front baada ya kusafishwa na Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa
kushirikiana na kampuni ya usafi ya Green Waste Pro.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency na wafanyakazi
wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd wakibadilishana mawazo baada ya
kuhitimisha zoezi la kusafisha fukwe za Kivukoni Front na kuishukuru kampuni ya
Green Waste Pro kwa kuitikia wito.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Hyatt Regency na
kampuni ya Green Waste Pro baada ya zoezi la usafi.
Post a Comment