Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II
(wapili kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo na kiongozi huyo ikulu jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Askofu wa Mwanza na Bukoba Askofu Jeronymos. Nyuma ya
Rais mwenye tai nyekundu ni mwenyekiti wa Hellenic society of Tanganyika
Dimitris Mantheakis, na kulia ni askofu mkuu wa Dar es Salaam na mashariki
askofu Dimistrious
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Kiongozi wa Kanisa la
Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kiongozi huyo wa
Kanisa la Orthodox yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo
mengine atatembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na kanisa hilo hapa nchini
ikiwemo Zahanati na shule ya msingi Iringa pamoja na Hospitali ambayo
inaendelea kujengwa huko Bukoba Mkoani Kagera.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi
wa Kanisa la Orthodox Pope Theodoros II ikulu jijini Dar es Salaam.Picha na Freddy Maro-IKULU
Post a Comment