Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya
Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata
ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (wapili kutoka kulia)
akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili
kutoka kushoto), Mkuu wa Magereza nchini, Kamishna Jenerali John
Minja (kulia) pamoja na maofisa mbalimbali kutoka nchini na Kenya, wakiingia
ndani ya kiwanda hicho.
Mshauri Mtaalamu wa Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza
kofia ngumu katika Jeshi la Magereza, Alpherio Moris (kulia) akimuonyesha
Rais Mwai Kibaki moja ya kofia ngumu (Helmet) ambayo inatarajiwa kutengenezwa
na kiwanda cha magereza Ukonga hivi karibuni.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jeneral John
Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum ya kiti Rais Mwai Kibaki wa
Kenya.
Rais Mwai Kibaki (wa kwanza kutoka kulia aliyevaa
tai) akiwafurahia Askari Magereza na ofisa kutoka nchini Kenya wakiwa
wamekaa kwenye kiti cha wapendanao kilichotengenezwa na wafungwa kiwandani
humo.
Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiwa na maofisa
mbalimbali wakiondoka Kiwanda cha Magereza Ukonga baada ya kumaliza
kuangalia vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Rais Mwai Kibaki akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi mbalimbali nchini pamoja na maofisa kutoka nchini Kenya.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Post a Comment