Matumaini (katikati)
akisaidiwa na wasanii wenzake muda mfupi baada ya
kutua.
Bi. Mwenda akiwa
amembeba Matumaini mgongoni.
Matumaini (kulia) akiwa
na Bi. Mwenda (wa pili kushoto) na anayefuata (kushoto) ni msanii mwenzake
Kiwewe wakisubiri gari la kumpeleka
hospitali.
Askari wakiwaelekeza
wasanii kukaa upande mmoja ili apate
hewa.
Matumaini akiwa amebebwa
mgongoni na msanii mwenzake, Mariam Athuman ‘Kalunde’ akimpeleka kwenye
gari.
Mama mkubwa wa Matumaini, Bi. Elizabeth (kushoto) na
Matumaini (katikati) wakiwa ndani ya gari tayari kuelekea hospitali ya
Amana.
Rais wa Shirikisho la
Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza na wasanii maeneo ya Amana
wakati Matumaini akiwa kwa daktari.
-----------
MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa
nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii
wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda
mrefu. Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.
credit: Global
Post a Comment