WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika matokeo hayo
yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa
kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati
wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo
Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government
Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia
masuala ya elimu.
Wadau wengine watatoka
Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Amesema Serikali inawaomba
wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa
Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa
ufanisi
Post a Comment