Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MWANRI APATA USAJIRI WA CHF ILIYOBORESHWA

N:Waziri Mwanri, akielekezwa kujisajili kitambulisha cha CHF iliyoboreshwa. Nyuma niMkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Mchimbi, mwakilishi wa Vodacom Bi. Kamhanda na Meneja wa Mradi wa HPSS,
N:Waziri Mwanri, akionyesha kitambulisha cha CHF iliyoboreshwa mara baada ya kukabidMkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Mchimbi.
N:Waziri Mwanri, akipokea kitambulisha cha CHF iliyoboreshwa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Mchimbi. Katikati ni Mwakilishi wa Vodacom Bi Kamhanda na kulia ni Meneja Mradi wa HPSS, Bw. Manfred Stoemer toka HPSS ya nchini Uswis
N:Waziri Mwanri, akipokea kitambulisha cha CHF iliyoboreshwa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Mchimbi. MradI unafadhiliwa na SDC na kutekezwa na HPSS ya nchini Uswisi..
Naibu Waziri Mwanri, akipigwa picha ya kitambulisho cha CHF iliyoboreshwa wakati wa Hafla ya Uzinduzi iliyofanyika leo, Dodoma Hotel, Dodoma.
Swiss Centre for International Health
Muongozo kwa Vyombo vya Habari
Uzinduzi wa Mfumo mpya wa Menejimenti ya Taarifa za Bima (IMIS) kwa
ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa)
katika Mkoa wa Dodoma
Leo tarehe 16 Februari, 2013 hapa Dodoma Mfumo mpya wa Menejimenti ya
Taarifa za Bima unaotumia teknolojia ya kisasa zaidi ya uwasilishaji
wa taarifa kwa kutumia simu ya mkononi na utunzaji wa kumbukumbu
umezinduliwa, ambao utasaidia kuwa na njia rahisi na ya haraka ya
kushughulikia madai yanayowasilishwa na vituo vya kutolea huduma baada
ya kuwahudumia wagonjwa wa CHF.
Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi iliyofanyika kwenye hoteli
ya Dodoma Hotel mjini Dodoma leo, Bw. Manfred Stoermer; Meneja wa
Mradi wa Health Promotion and System Strengthening Project HPSS
amesema, “mabadiliko haya ni sehemu ya jitihada kubwa zinazojulikana
kama Health Promotion and System Strengthening (HPSS) Project au Mradi
wa Tuimarishe Afya, ambao ni sehemu ya ushirikiano wa kimaendeleo kati
ya Tanzania and Uswisi.”

Bw. Stoermer anaendelea kusema “Kwa kutengeneza na kuanzisha mfumo wa
IMIS, Mfuko wa Afya ya Jamii sasa una suluhisho kamambe la utunzaji wa
taarifa, ikiwa ni pamoja na uandikishaji wa wanachama kwa kutumia
teknolojia ya simu ya mkononi, menejimenti ya michango, ushughulikiaji
wa madai na ulipaji, pamoja na ukusanyaji wa mrejesho wa wanachama
(member feedback collection). Kuiwezesha bima ya afya vijijini nchini
Tanzania kuwa na mfumo wa utunzaji taarifa kutasaidia sana uwezo wake
wa kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi”

Mfumo wa teknolojia ya Mawasiliano na Habari (IT) utaruhusu ufanyaji
kazi kukiwa na mtandao au bila mtandao. Upatikanaji wa kadi ya CHF kwa
kila mwanakaya- ambapo awali kadi moja ilikuwa ikitolewa kwa kaya-
mfumo wa IT utamuwezesha kila mwanachama kupata huduma za afya katika
kituo chochote cha kutolea huduma ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Katika CHF iliyoboreshwa tatizo moja kubwa mpaka sasa, la kuwatambua
wanachama maeneo ya vijiji katika vituo vya kutolea huduma vilivyopo
katika vijiji vingine litakuwa limetatuliwa. Kila kituo cha kutolea
huduma kilichopo kwenye mtandao wa CHF kimepokea simu maalumu
(zinazopatikana Tanzania) inayoweza kuunganishwa na mfumo wa taarifa
wa CHF na kupakua (download) picha za wanachama kutoka kwenye mfumo wa
IT, ambapo inawezesha kumtambua mwanachama kwa haraka. Kadi ya CHF
iliyoboreshwa inaweza kutumika katika kituo chochote cha kutolea
huduma katika wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, pamoja na hospitali. Kwa
mfumo huu mpya, uandikishaji wa wanachama ni wa haraka na rahisi
kwakuwa Maafisa Uandikishaji wapo katika ngazi ya vijiji na mitaa kwa
ajili ya kuwaandikisha wanachama kwa kutumia simu ya CHF.

Simu hizo pia zinatumika kuwaandikisha watu kwenye CHF kwa kuwapiga
picha na kuziwasilisha kwenye mfumo wa kumbukumbu (database) wa IMIS.
Yote haya yanaweza kufanyika hata kwenye maeneo ya vijijini yenye
shida ya mtandao kwa kuwa mfumo unaruhusu kutunza kumbukumbu
zinazochukuliwa wakati hakuna mtandao.
Mradi unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) na
unatekelezwa na Taasisi ya Swiss Tropical and Public Health Institute
(Swiss TPH), Uswisi, na Taasisi wadau, the Micro Insurance Academy
(MIA), Ujerumani, kwa ushirikiano na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI),
Tanzania. Mfumo wa IT umetengenezwa na Kampuni iliyopo Dar es Salaam
inayojulikana kama Exact Software Company na wataalamu kutoka kwenye
Mradi wa HPSS.

Vodacom Tanzania inasaidia mradi kama mdau muhimu kwenye masula ya
mawasiliano. Katika awamu hii ya utengenezaji wa mfumo na majaribio
mpaka Januari 2015 Vodacom inatoa huduma ya bure ya internet na
mawasiliano ya ujumbe wa maandishi kati ya kompyuta kuu na vituo vya
kutolea huduma na maafisa uandikishaji wa CHF waliounganishwa na
mtandao wa CHF.

“Vodacom inajivunia kwa mara nyingine kuwa mstari wa mbele kwa matokeo
mazuri kwenye masuala ya afya. Tumejizatiti kuendelea kuwekeza kwenye
teknolojia inayohitajika na ambayo itawasaidia wataalamu kufanya kazi
zao kwa ufanisi zaidi. Hii ndio maana ya kuwaunganisha watu na
kubadilisha maisha kwa mujibu wetu sisi Vodacom.”Anasema Mkuu wa
kitengo cha mawasiliano na mahusiano cha Vodacom Joseline Kamuhanda

Utengenezaji wa mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu (IMIS) ulifanyika kwa
kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, na Bima ya
Afya ya Taifa ili kukidhi vigezo na kuwa na uwiano na mifumo ya IT ya
Serikali za Mitaa. Mfumo mpya wa CHF, umeundwa katika hali ambayo
unaweza kusambazwa na kutekelezwa kwa urahisi nchi nzima, mara baada
ya kujaribiwa na kuthibitika kuwa na ufanisi katika Mkoa wa Dodoma.

Mawasiliano:
Prof. M. Meshack
Kiongozi wa Mradi wa HPSS
P.O.Box 29, Jengo la Tanesco
Eneo la Jamatini, Dodoma
Tel
+255 26 2323 084
Mfadhili:
Swiss Agency for Development and Cooperation (SDC)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top