WAWAKILISHI
pekee wa Tanzania timu ya Azam Fc, leo tena imeendelea kufanya vizuri
katika mchezo wake wa Kombe la Shirikisho, baada ya kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya BYC II ya Lyberia, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja
wa ATS, Jijini Monrovia. Mchezo huo ni wa kwanza ambapo Azam imejiweka
katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri katika mchezo wake wa marudiano
unaotarajia kupigwa hapa nyumbani hivi karibuni. Hadi timu hizo
zinakwenda mapumziko Azam ilikuwa tayari imelala kwa bao 1-0, ambapo bao
la kusawazisha na la kuongoza yalipatikana katika kipindi cha pili.
Loading...
Post a Comment