Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
akiwakatika mazungumzo na Mjumbe wa Tume ya Uongozi wa Taifa wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC), Liu Yunshan, kwenye Ofisi za chama hicho mjini
Beijing China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwakatika
mazungumzo na Mjumbe wa Tume ya Uongozi wa Taifa wa Chama Cha Kikomunisti cha
China (CPC), Liu Yunshan, kwenye Ofisi za chama hicho mjini Beijing China.
Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Picha na Bashir
Nkromo-China
--
NA BASHIR
NKOROMO, BEIJING, CHINA
KATIBU Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema Tanzania kuna wawekezaji
katika sekta mbalimbali za uchumi, lakini Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba
wawekezaji walio wakubwa zaidi kwa tija ni wakulima.
Kinana alisema
hayo Machi 20, 2013, wakati akizungumza na Mjumbe wa Tume ya Uongozi wa Taifa wa
Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Liu Yunshan, mjini hapa, akiwa katika
ziara ya kimafunzo nchini China, ambayo anafanya kwa mwaliko wa chama cha CPC,
na amefuatana ujumbe wa watu 14 wakiwemo viongozi waandamizi na maofisa wa
CCM.
Kinana alisema,
kutokana na kutambua mchango mkubwa katika kuweza kuinua uchumi wa Tanzania,
serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imeanzisha na kuusimamaia mpango wa Kilimo
Kwanza kwa lengo la kuwezesha wakulima walio wengi kuchangia uchumi wa taifa
kupitia uwekezaji katika sekta hiyo na hiyo pia kuinua hali za vipato
vyao.
Alisema, ili
kupata mafanikio zaidi na ya haraka, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi itautumia
uzoefu wa jinsi Chama Cha Kikomunisti cha kilivyoweza kuratibu na kusimamia kwa
hali ya juu miradi ya kilimo hadi kuiwezesha China kuinuka kiuchumi njia kuu
ikiwa ni kupitia sekta ya kilimomo.
Kinana alisema,
alimwambia Liu, kwamba, Chama Cha Mapinduzi kinaona umuhimu wa kuiga uzoefu wa
China katika kukuza uchumi kwa kuwa misingi ya kisiasa na na sera za Tanzania na
nchi hiyo katika uchumi zinafanana kwa kuwa zinalenga zaidi kunua hali za
wanyonge ambao ni wajasiramali wadogo wadogo katika uwekezaji kwenye shughuli
mbalimbali na kilimo.
Alisema, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kinakaribisha
mataifa ya nje ikiwemo China kushiriki katika uwekezaji, lakini akabainisha
kwamba uwekezaji ambao Tanzania inahitaji zaidi ni ule utakaonufaisha pande
zote, Tanzania na nchi itakayohusika na kwamba baadhi ya faida ambazo inatarajia
Tanzania kuzipata ni uwekezaji ambao utatengeneza nafasi nyingi za ajira kwa
Watanzania.
Kuhusu siasa za
nje, Kinana aalimwambia Liu kuwa, Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza kama chama
tawala, kwa kwamba Tanzania ni nchi huru hivyo haichaguliwi rafiki bali yenyewe
ndiyo inayochagua kulingana na faida ambayo Watanzania wataipata, na haitafuata
msukumo au mapendekezo ya taifa lolote la nje na kusisitiza kwamba Tanzania na
China zina urafiki wa kihistoria tangu wakati wa harakati za ukombozi wa nchi
za kusini mwa Afrika.
"Na tutaendelea kuundumisha urafiki huu wa kindungu
ulioanzishwa na waasisi wa mataifa yetu, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa
upande wa Tanzania na hayati Mao Tsetung kwa upande wa China", alisema Kinana na
kuongeza;
"Tunaamini
Tanzania inayo mengi ya kujifunza kutoka China kama ilivyo China nayo kuwa na
mengi ya kujifunza kutoka Tanzania, tunaamini ziara ya Rais wa China Xi Jinping
nchini Tanzania, itakayoanza (Jumamosi), mara baada tu ya kuchaguliwa rasmi kuwa
rais wa nchi yake, ni alama muhimu ya namna chama cha kiongozi huyo ambacho yeye
ni Katibu Mkuu, kinavyothamini uhusiano wake na CCM na Watanzania kwa
jumla.
Alisema, kauli aliyotoa Rais Ping katiba Bunge Kuu la
China, inayosisitiza nchi hiyo kuendelea kupambana na umasikiniu, kuondoa
urasimu na umangimeza, kuimua hali za wananchi na kudumisha amani duniani
inastahili kupongezwa na kila mpenda maendeleo duniani kote.
Kwa upande
wake, Liu katika mazungumzo hayo, aliipongeza CCM kwa namna inavyoongoza,
uongozi ambao amesema kutokana na umadhubuti umeweza kuifanya Tanzania kupiga
hatua ya kubwa kiuchumi na kisiasa ambapo nchi imeendelea kuwa ya amani na
utulivu na kuahidi CPC kuendeleza na kuimarisha uhusiano na CCM kwa manufaa ya
serikali ya Tanzania na wananchi kwa jumla.
Alisema Tanzania chini uongozi wa Mwenyekiti wa CCM,
Rais Jakaya Kikwete, imeweza kupiga hatua kubwa ingawa bado zipo changangamoto
nyingi za kushughulikiwa na kueleza imani yake kwamba chini ya Rais Kikwete
Tanzania itanedelea kuwa Umoja, amani na mshikamano vitasaidia kuleta maendeleo
zaidi Tanzania.
Kiongozi huyo
aliasa kuwa upo umuhimu wa kuimarushwa Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee
kupambana na uninafsi, kujenga uaminifu na kutumikia wananchi kwa kufuata
misingi mikuu ya uongozi bora. " pia nakupongeza mheshimiwa Kinana kwa kuteuliwa
kuwa katibu Mkuu wa Chama, naamini kuteuliwa kwako kumezingatia mchango mkubwa
uliokwishatoa kwa taifa la Tanzania na uchapakazi wako.
Post a Comment