
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(Tucta)
---
Dar es Salaam: Siku chache baada ya Mwenyekiti wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Ayoub Omar kuvuliwa wadhifa wake,
imebainika kuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Nicolaus Mgaya naye amenusurika
kung’olewa kwenye wadhifa wake.
Mgaya aliliambia Mwananchi jana kuwa njama za kumng’oa kwenye wadhifa huo zilipangwa na wapinzani wake ambao walitoa hoja dhaifu bila ushahidi kuwa ana uhusiano wa wanawake (hawakutajwa).
“Hoja zao hazikuwa na maana, walikuwa wakihisi tu kuwa natembea na mwanamke fulani bila kuwa na ushahidi, pia suala hilo halihusiani na utendaji wangu wa kazi,” alisema Mgaya na kuongeza:
“Unajua katika umoja wowote lazima kuwe na majungu watu wanaweza kuwa na sababu zao nyingi tu, hivyo sikuona ajabu niliposikia nafanyiwa zengwe.”
Alisema hoja za kutakiwa kung’oka zilijadiliwa na kumalizwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichomalizika juzi, ndiyo maana hazikuibuka tena katika kikao cha Baraza Kuu la Tucta kilichomalizika jana jioni. Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea.......>>>>


Post a Comment