Na Mroki Mroki-Father
Kidevu Blog-Moshi
Wanariadha kutoka Nchini
Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro
Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro.
Wakenya
walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao Kipsang
Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za mwaka huu upande wa
wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya
Dhahabu.
Nafasi
ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo
Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri, Frida Too,
Rosaline David na Jane Kenyara.
Aidha katika mbio za
Kilometa 21, Kenya ilitamba tena kwa upande wa wanaume baada ya wakimbiaji wake
watatu kushika nafasi za juu ambapo Mshindi alikuwa ni Silah Limo huku nafasi ya
pili ikienda kwa Bernard Kiprotich na nafasi ya tatu ikienda kwa Charles
Ogari.
Mtanzania Dickson Marwa
alinyakua nafasi ya nne na nafasi za tano na sita zikenda Tena Kenya kwa
wakimbiaji Peter Kusgei na Evans Taigey nafasi ya saba ilishikwa na Mtanzania
Stephano Huche na kuporwa tena na Kenya nafasi ya nane iliyoenda kwa Patrick
Wambugu aliyekimbia mbele ya watanzania wawili waliofunga hesabu ya wakimbiaji
kumi bora ambapo namba tisa alikuwa Said Makula na kumi alikuwa Peter
Sule.
Shangwe ya watanzania
iliibuliwa na Mwana dada Sara Makera Ramadhan baada ya kunyakua medali ya
dhahabu kwa kuibuka mshindi wa kwanza mbele ya mkenya Vicomi Chepkemoi huku
nafasi ya tatu ikichukuliwa na mtanzania mwingine Failuna
Makanga.
Nafasi
ya nne ilienda kwa Joyce Kiplimo wa Kenya aliyefuatiwa na mwenzake Pauline
Muchiri kasha Mtanzania Catherine Tuku alishika nafasi ya sita na zilizosalia
hadi nafasi ya kumi zikienda kwa Nchi ya Kenya ambao ni Nancy Kotch, Jacinta
Mboani, Florence Cheruiyot na Phylas
Jelagat.
Jumla
ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon
2013.
Wakimbiaji wa Kenya
wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio
hizo.
Mfukuza Upepo kutoka Nchini
Kenya na Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika Mbio za Kilimanjaro Marathon
akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika
Mjini Moshi.
Eunice Muchiri akikimbia na
kumaliza wapili mbio za Kilimeta 42 Wanawake, katika Mbio za Kilimanjaro
Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha
Ushirika Mjini Moshi.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio
za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na kuwa
kocha wa Kwanza wa Timu ya Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa kwake
miaka 10 iliyopita.
Wakimbiaji mbalimbali
wakishiriki katika mbio hizo leo mkoani
Kilimanjaro.
Post a Comment