Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINANA NA UJUMBE WAKE WAENDELEA NA ZIARA YA KUIJENGA ZAIDI CCM KIMATAIFA HUKO NANCHONG, NCHINI CHINA


1A
 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akiwasalimia wazee katika kijiji cha mradi wa wakulima wa kupunguza umasikini cha Nanchong, jimbo la Sichuan, China, alipotembelea kijiji hicho, Machi 16, 2013. Anayemsalimia ni Ning Xiu (78). Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo) 1B
 
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu shughuli za kilimo alipotembelea mji wa Dantong, Nanchong kwenye miradi ya kilimo kwa ajili ya kupambana na umasikini, Machi 16, 2013. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo) 3
 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China, jimbo la Sichuan, Zhang Ning, wakitazama kazi za watoto, katika shule ya awali katika kijiji cha Dantong, wilaya ya Nanchong, Kinana na ujumbe wake walipotembelea miradi ya kilimo kwa ajili ya kupunguza umasikini, katika kijiji hicho, Machi 16, 2013.Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo) 4
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi, akitazama vifaa vya michezo ya watoto katika shule ya awali ya Kijiji cha Dantong, jimbo la Sichuan, Msafara wa Kinana ambao Amina yumo, ulipotembelea kijiji hicho kuona shughuli za mradi wa kilimo wa kupunguza umasikini, Machi 16, 2013. Kinana yupo China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro, na Watatu kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Khadija Aboud. (Picha na Bashir Nkoromo) 5
 
Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama moja ya mashamba makubwa ya wakulima walipo kwenye mradi wa kupunguza umasikini, katika Kijiji cha Dantong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya nyanja mbalimbali za kimaendeleo, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo cha CPC. (Picha na Bashir Nkoromo).
6
 
Wakulima Kijiji kinachoendesha mradi wa kupambana na umasikini wa kilimo cha Nanchong, jimbo la Sichuan, wakiwa kazini Machi 16, 2013. 7.
 
KILICHO CHA AINA NTAKIPELEKA MKOANI KWANGU”, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema wakati akiwa kando ya shamba la kisasa la njegere, katika kijiji cha Nanchong, Jimbo la Sichuan, China, Machi 16, 2013. Jesca yupo katika msafara wa viongozi 14 wa CCM unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana nchini China. 8
 
Shamba la kabichi katika kijiji cha Nanchong, jimbo la Sichaun, China, Shamba hilo lipo katika mradi wa kupunguza umasikini katika kijiji hicho unaofanywa na serikali ya Jimbo la Siachuani ya Chama Cha Kikomunisti cha China. (Picha zote na Bashir Nkoromo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top