Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAANDAMANO YA KUMTAKA WAZIRI WA ELIMU AJIUZURU JESHI LA POLISI MWANZA NAYO YAIPIGA STOP CHADEMA.

 


Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limepiga marufuku maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika siku ya jumatatu kumshinikiza Waziri wa Elimu ajiuzuru kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa mwaka 2012.

Akitoa taarifa leo asubuhi katika ofisi za jeshi hilo mkoani Mwanza Kamanda wa polisi mkoa Ernest Mangu amesema kuwa jeshi lake limeyazuia maandamano hayo kwa sababu za kimsingi za usalama. (Bofya play kumsikiliza)

Akizitaja sababu hizo kamanda Mangu amesema kuwa suala la matokeo ya kidato cha nne kuwa mabaya serikali tayari imeliundia tume ambayo bado inaendelea kukusanya maoni kwa wananchi hivyo haoni sababu za CHADEMA kufanya maandamano na kuwataka viongozi wake kuwasilisha hoja zao wanazodai kuwa za msingi kwenye tume husika na si kufanya maandamano yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani.
Kwa mkoa wa Mwanza CHADEMA ilitoa taarifa za kufanya maandamano katika wilaya za Sengerema, Misungwi na Magu.

Mangu ameongeza kuwa jumatatu ni moja kati ya siku za kazi na shughuli mbalimbali za biashara hivyo kufanya maandamano kwenye viunga mahali kokote ni chanzo cha kuzuia shughuli za uzalishaji na biashara kufanyika kwa ufanisi kwani wadau watafunga shughuli zao wakihofia uporaji na usalama wa mali zao.

Tayari jeshi la polisi Mwanza limepokea taarifa ya makundi mbalimbali kuibuka na kudai kuyapinga maandamano hayo wakiwemo wafanyabiashara walioko katikati ya jiji wakisema kuwa yatasababisha huduma zao kusimama.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top