Mbunge wa Chambani, Salim
Hemed Khamis amezikwa kijijini kwake Mizingani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Sief
Sharif Hamad aliongoza mamia ya wananchi kwenye
mazishi
hayo.
Awali, Rais
Jakaya Kikwete aliongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuaga mwili wa Mbunge
wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF) kwenye viwanja vya Karimjee, aliyefariki
dunia juzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Akitoa salamu
za Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),
William Lukuvi alisema Bunge limepoteza mtu shupavu ambaye alikuwa mchangiaji
mzuri kwa kutoa hoja zenye lengo la kujenga.
Alisema licha
ya kuwa mbunge wa upinzani, lakini hoja zake zililenga kukosoa Serikali na
kurekebisha na kwamba, pale alipobaini upungufu na daima
hakusita.
Akizungumza
kwa niaba ya familia, Mbunge wa Mtambilem Masoud Salim alisema Serikali zote
mbili na uongozi wa Bunge wamefanya kazi mzuri kuanzia hospitali hadi maziko
yake.
Mwenyekiti wa
CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema chama chake kimepoteza kiongozi na
mwanachama mzuri na kwamba, itakuwa vigumu kuziba pengo
hilo.
Mazishi hayo
pia yalihudhuriwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Mambo ya Nje, Edward Lowassa na viongozi mbalimbali.
Awali,
viongozi waliohudhuria kutoa heshima za mwisho mjini Dar es Salaam, ni Makamu wa
Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Wilibrod Slaa na wabunge mbalimbali.
Akisoma
historia fupi ya marehemu Khamis, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema
kulingana na taarifa za madaktari alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la
damu.
source::MWANANCHI:::

Post a Comment