*Aagiza polisi iwachukulie hatua stahiki
wahusika
*Awataka wakuu wa mikoa, wilaya kusimama kidete
RAIS Jakaya Kikwete ameonekana kuchoshwa na vitendo vya uchochezi wa kidini vinavyoendelea nchini, baada ya kuliagiza Jeshi la Polisi liwachukulie hatua stahiki watu wote wanaohusika ili liwe fundisho kwa watu wengine.

Rais Kikwete
alitoa kauli hiyo juzi usiku, wakati akihutubia taifa katika utaratibu wake
aliojiwekea kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi
“Nimewakumbusha polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika.
“Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao “ajizi nyumba ya njaa”, alisema Rais Kikwete.
Alisema wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini wasipodhibitiwa ipasavyo, wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia.
“Nimewakumbusha wakuu wa wilaya na mikoa kama walinzi wa amani wa maeneo yao ya uongozi, watimize ipasavyo wajibu wao,” alisema Rais Kikwete.
Kutokana na hali hiyo, amewataka Polisi wakamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Alisema anaendelea kuwasiliana na viongozi wa dini kwa ajili ya kuzungumza nao juu ya wajibu wao wa kuhakikisha wafuasi wao hawawi chanzo au sehemu ya tatizo na mifarakano miongoni mwa waumini wa dini nyingine.
Alisema kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka wa jana, kumekuwepo na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
Alisema miongoni mwa matukio hayo, ni pamoja na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje.
“Kumekuwepo na matumizi mabaya ya redio na simu za mkononi na mifumo mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini zetu hizi kubwa hapa nchini. Kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama ilivyotokea Buseresere mkoani Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar.
“Watanzania hatujawahi kuwa hivi, kumetokea nini? Miaka yote Watanzania ni watu tunaotambua na kuheshimu tofauti za dini zetu mbalimbali tunazoabudu. Watanzania ni waelewa na kwa ajili hiyo, tumekuwa tunavumiliana kwa tofauti zetu na ndiyo maana tumekuwa tunaishi pamoja kidugu, kwa umoja na kushirikiana kwa mambo yote yanayotuhusu maishani, isipokuwa wakati kila mmoja anapoingia kwenye nyumba ya ibada kumuomba Mola kwa misingi na taratibu ya dini yake.
Kuhusu matokeo ya kidato cha nne mwaka huu, Rais Kikwete ameonyesha masikitiko kutokana na matokeo kubwa mabaya zaidi.
Alisema hatua sahihi zisipochukuliwa, hali inaweza kuwa mbaya zaidi siku zijazo.
“Nimeshtushwa na matokeo haya, lazima tutafute sababu nini na tusipofanya hivyo, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi na lawama zinaweza kuwa kubwa zaidi kwa Serikali,” alisema Rais Kikwete.
“Isitoshe, kiwango cha ufaulu wa vijana kimepungua, mwaka 2010 wanafunzi 10 bora wote, walikuwa wamefaulu daraja la kwanza la alama au pointi 7. Mwaka 2011 katika wanafunzi 10 bora wanane walipata daraja la kwanza kwa alama 7 na wawili alama 8. Mwaka 2012 katika wanafunzi 10 bora, watatu walipata daraja la kwanza kwa alama 9, watatu alama 10 na wawili alama 7,” alisema Rais Kikwete.
Alisema ufaulu huo, unazua maswali kwa watu wengi ambao wanahitaji kupatiwa majawabu ya uhakika.
“Kulikoni mwaka 2012? Ndiyo msingi wa uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuamua kuunda tume ya kuliangalia suala zima la mitihani ya mwaka 2012 na matokeo yake. Hali hii haijawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.
“Ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo lazima ukweli wake ujulikane kwa uhakika. Hii itawezesha Serikali na wadau wengine kuchukua hatua stahiki kurekebisha mambo mapema iwezekanavyo, ili hatimaye mambo yawe mazuri siku za usoni,” alisema Rais Kikwete.
Alisema hivi sasa kunatolewa mawazo lukuki kuhusu sababu za kwa nini matokeo yamekuwa mabaya, huku watu wakifikiri lipo tatizo katika utungaji wa mitihani, usahihishaji au kutoa maksi kwa watahiniwa kidogo.
“Wapo wanaodhani walimu hawawajibiki ipasavyo au baadhi yao kutokumudu masomo wanayofundisha. Wapo wanaofikiria kuwa wanafunzi hawako makini katika kufuatilia masomo na wazazi hawajali kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni. Wapo wanaoinyooshea kidole Serikali kwa sera, mitaala na uwekezaji usiokidhi mahitaji ya maendeleo ya elimu. Wapo wanaofikiria kuwa Serikali kushindwa kuongeza mishahara ya walimu kwa asilimia 100, kama walivyotaka imechangia,” alisema Rais Kikwete.
Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete amemtaka kila mtu mwenye mawazo ambayo anafikiri yanafaa ayafikishe kwenye tume pindi itakapoundwa na kuanza kazi.
Kuhusu suala la amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rais Kikwete alisema hatua kubwa za kufikia amani zimefikiwa, ikiwa ni pamoja na Tanzania kupeleka kikosi cha askari wa kulinda amani.

mtanzania
Post a Comment