Ridhiwani Kikwete
--
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yusuf
Manji leo amemtambulisha Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi
wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya Mafia/Nyamwezi eneo
la Ilala jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo
makao makuu ya klabu yaliyopo mtaa wa Twiga na Jangwani, Manji alisema uteuzi wa
Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake ya uwakili, na moyo alionao
katika kujitolea katika kazi mbali mbali za klabu ya Yanga.
"Wote tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga
kwa muda mrefu, amekua akijitoa katika kazi mbali mbali za maendeleo ya klabu,
hivyo tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta
maendeleo ya klabu" alisema Manji
Katika kamati hiyo ambayo Ridhiwani ameteuliwa , amepewa
fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega
uchumi hicho katika mtaa wa mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au
kupunguza kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.
Mara
baada ya kutambulishwa kwa wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema
anashukuru kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na
kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo
unafanikiwa.
"Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza
kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi wa
kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo litasaidia katika
uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani
Aidha Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia
kimekuwepo kwa mda mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini
tutajitahidi ili kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na
kuwa sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.
Ridhiwani
mwisho alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu
bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga sehemu mbali
mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo yatasaidia katika kuendeleza
uchumui wa klabu.
Post a Comment