Taarifa za ndani kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ni
kwamba kikao cha serikali kupitia wizara ya habari na michezo na shirikisho la
soka nchini kuzungumza juu ya suala la serikali kuondoa usajili wa katiba mpya
ya TFF kimeishia kwa serikali kuliagiza shirikisho hilo kuwataarifu wanachama
juu ya mkutano mkuu ndani ya siku 5 zijazo, na kuandaa mkutano wa
kufanya mabadiliko ya katiba katika kipindi cha siku 40 zijazo kutoka
leo.
Kwenye kikao hicho TFF
iliwakilishwa na Katibu Mkuu Angetile Osiah, mwanasheria Alex Mgongolwa, Wallace
Karia na Mkurugenzi wa michezo Sunday Kayuni - taarifa za kutoka ndani ya kikao
hicho zinasema kwamba TFF ilionekana haikufuata taratibu za kufanya marekebisho
ya katiba na hivyo serikali ikafikia maamuzi ya kuwaagiza waandae mkutano mkuu
wa wanachama wote wa TFF ili kukidhi matakwa ya kufanya marekebisho ya
katiba.
Pia baada ya kufanyika
kwa mkutano mkuu, serikali imeagiza uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo ufanyike
katika kipindi cha siku 40 baada ya mkutano mkuu kufanyika.
SOURCE
SHAFFIHDAUDA

Post a Comment